Babumawe
JF-Expert Member
- Sep 12, 2014
- 2,556
- 2,571
Kuna mama mmoja hapa kitaani yeye ni mjamzito sasa huwaga kila nikipita lazima anisimamishe, siku ya kwanza nimepita akanisimamisha akaniuliza unatumia deodorant gani basi pasipo shari mimi kwa upole na unyenyekevu nikamjibu baada ya hapo basi nikapita zangu kushoto nikaendelea na mwendo.
siku ya pili nikapita tena akanisimamisha nikasimama kumsikiliza anataka kunambia nini akaja kwa kasi sana akanambia hataki kuniona nikipita mazingira yale, nikamuuliza kwanini hataki nipite wakati ile ni njia na kila mtu anapita, akanambia hapendi kusikia harufu ya deodorant yangu, nikamsikiliza tu mwishowe sikumjibu kitu nikaondoka zangu.
sasa jana jioni napita maeneo yale akanijia kwa lengo la kunivamia huku uso akiwa ameukunja kwa hasira huku ananambia si nilikuambia sitaki upite maeneo haya, hutaki kunisikiliza hivyo utanisikiliza kwa vitendo leo akaokota jiti kutaka kunipiga nalo, hakika nilitahamaki kwani ni tukio ambalo sikutarajia kama lingeweza kutokea, nikawa namtuliza akawa hanisikii basi nikajawa na hasira sana nikamkamata shingo kwa hasira huku namwambia ukiendelea na vurugu zako basi nakunyofoa shingo hii.
Bahati mzuri lile eneo lilikuwa karibu na kwao wakaja watu na ndugu zake pale basi wakasuluhisha huku wakinambia kuwa huyu mtu ndo alivyo akiwa na mimba anafanyaga vitu vya ajabu. Wakanambia muda mwingine hata muda wa kula anachukua sahani yake anakwenda kukaa mlango wa chooni ndo anakula yaani anapenda kusikia ile harufu ya mavi. Kwakweli nilinyong'onyea kusikia vile kwa maana wangechelewa kidogo tu sijui ingekuwa inaongeleka kitu gani sasa.
using JamiiForums mobile app