View attachment 2414204
Hawa jamaa walinifuata Insta na kutaka nifanye nao kazi ya ugavi. Walijitambulisha kuwa ni Sasakawa Lodge ndani ya Serengeti. Wakasema walitembelea trade profile yangu wakasema tukutane next day evening huko Serengeti tuingie mkataba.
Nikapigiwa na mwanamke ambaye anazungumza kiingereza cha lafudhi ya nchi jirani akinielekeza kuwa nikifika wameniwekea reservation na watanirfund nauli. Nikaulizia how will I get there akasema nikifika Arusha kuna flight shuttlels za kubeba watalii nitatumia hizo ndege.
Baadaye kidogo akanipigia kunijulisha kuwa kuna ndege ya TANAPA inatokea Zanzibar ina nafasi ya mtu mmoja hivyo ameongea na pilot amemkubalia kunichukua. Akanitumia namba nikacheki na rubani ambapo alinitajia kiwango cha nauli akisisitiza nimtumie kwa mobile money. Nimpe majina yangu anitumie flight pass.
Tangu awali nilishaanza kunusa utapeli. Nikamrudia yule mdada kumweleza yote na kumuuliza,kwa nini wao wasimlipe rubani mimi nikapanda ndege nikaja? Akasema utaratibu wao ni kutoa refund na kama ninataka deal basi nijigharimie kwenda watanirudiahia nauli na watanipa ya kurudia.
Kuna watu kama wanne hivi nimekuta wanalalamika nyakati tofauti kuhusiana na hii kampuni...
Naweka screenshots za mawasiliano
View attachment 2414207
TANAPA jina lao linatumika kutapeli, lakini mamlaka ta Mawasiliano badala ya kushughulika na hawa wahalifu badala yake wanadukua nani kamsema kiongozi