Almas Kasongo: Bodi ya ligi itatoa adhabu kwa Maofisa Habari wa timu wanaochekesha na kushindwa kuzungumzia Mpira

Almas Kasongo: Bodi ya ligi itatoa adhabu kwa Maofisa Habari wa timu wanaochekesha na kushindwa kuzungumzia Mpira

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almas Kasongo amesema msimu watatoa adhabu kwa Maofisa Habari wa timu wanaochekesha na kushindwa kuzungumzia Mpira huku akizikumbusha klabu kufuata kanuni kwa kuajiri maafisa habari wenye elimu ya habari.

“Kuna Muda unamsikiliza Ofisa Habari wa timu na kujiuliza, huyu ni kiongozi wa timu au mchekeshaji? Niseme tu ndugu zangu, msimu ujao tutadili na watu hawa kwa kuwapa adhabu” —— amesema Kasongo.
 
kuchekesha tu au kuna lingine au alichotaka kulisema kashindwa kuliweka ktk lugha nzuri akaona aseme 'kuchekesha'
 
Naweka mbele weledi katika kazi yeyote.

Ila soka letu bila kelele au vichekesho (sio matusi) vya hawa wasemaji na mashabiki hamna lolote.

Taratibu zifuatwe, ila sisi kwenye pitch bado sana.

Ni kelele tu zinatengeneza fans base kubwa katika soka letu.

Utaratibu huu ikifutwa:
1. Manara nampa wiki tu watamla kichwa.
2. Ahmed Ali miezi mitatu inamtosha, japo anabadilika badilika kulingana na upepo.
3. Ibwe nae anapaswa kujiangalia, haka kajamaa nako kana maneno machafu sana.

4. Ali Kamwe yupo safe kabisa katika hili.
 
Itakua Kasongo mpira umemshinda ndio wanaboronga huko TFF ina watu wasiojua mpira kabisaa kila wakiamka wanachoongea wanajua wao...
 
Utendaji Mkuu wa bodi ya ligi umemlevya, bora Angekaa kimya,
 
Tutawangezea pale na uchekeshaji. Wao waajiri maafisa wao wa bodi ya ligi
 
Siku huyo Kasongo na Bodi ya Ligi wakifuta huu utaratibu wa kuwa na wasemaji wa timu, na badala yake hilo jukumu likaachwa kwa makocha wa timu husika kama wafanyavyo wenzetu wa ng'ambo; mje mnishtue.

Ila kwa sasa niacheni tu niendelee kupiga usingizi. 😴
 
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almas Kasongo amesema msimu watatoa adhabu kwa Maofisa Habari wa timu wanaochekesha na kushindwa kuzungumzia Mpira huku akizikumbusha klabu kufuata kanuni kwa kuajiri maafisa habari wenye elimu ya habari.

“Kuna Muda unamsikiliza Ofisa Habari wa timu na kujiuliza, huyu ni kiongozi wa timu au mchekeshaji? Niseme tu ndugu zangu, msimu ujao tutadili na watu hawa kwa kuwapa adhabu” —— amesema Kasongo.
Msemaji wa timu ni mwajiriwa na siyo kiongozi.
 
hii yote wana msaka manara tu, no one else. Akiongea ujinga ban for 5 years or more.

just ask yourself why now??

yanga wanachafua brand mapema
 
Siku huyo Kasongo na Bodi ya Ligi wakifuta huu utaratibu wa kuwa na wasemaji wa timu, na badala yake hilo jukumu likaachwa kwa makocha wa timu husika kama wafanyavyo wenzetu wa ng'ambo; mje mnishtue.

Ila kwa sasa niacheni tu niendelee kupiga usingizi. 😴
ligi yetu kivyetu vyetu.

foreign managers can't use our local language also it improves the hype
 
Saf sana wale comedian wabaki kwenye comedi mpira n kwa ajili ya watu wa mpira
 
Back
Top Bottom