Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
NakaziaMpira ni burudani, kuizungumzia burudani sioni ubaya pakiwepo na vicheko, wachezaji wenyewe wanataniana uwanjani wanacheka kwanini sisi mashabiki tusicheke nje ya uwanja?!
Msemaji wa timu ni mwajiriwa na siyo kiongozi.Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almas Kasongo amesema msimu watatoa adhabu kwa Maofisa Habari wa timu wanaochekesha na kushindwa kuzungumzia Mpira huku akizikumbusha klabu kufuata kanuni kwa kuajiri maafisa habari wenye elimu ya habari.
“Kuna Muda unamsikiliza Ofisa Habari wa timu na kujiuliza, huyu ni kiongozi wa timu au mchekeshaji? Niseme tu ndugu zangu, msimu ujao tutadili na watu hawa kwa kuwapa adhabu” —— amesema Kasongo.
ligi yetu kivyetu vyetu.Siku huyo Kasongo na Bodi ya Ligi wakifuta huu utaratibu wa kuwa na wasemaji wa timu, na badala yake hilo jukumu likaachwa kwa makocha wa timu husika kama wafanyavyo wenzetu wa ng'ambo; mje mnishtue.
Ila kwa sasa niacheni tu niendelee kupiga usingizi. 😴