nusuhela
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 5,915
- 7,210
Naweza nikajiita loser. Niliutumia ujana wangu vibaya sana. Nilijiona mimi ndio mimi. Sikutaka kuwa na mahusiano ya kudumu. Nilipenda kupita bila kujali hisia za wale ninaowahitaji.
Nilijiona mimi bora kuliko wengine. Nikawadharau waliojitoa kwaajili yangu. Hakika nilijua kuchezea mioyo ya wanawake.
Japo sina mvuto, hela wala sikutokea kwenye familia ya kitajiri, lakini nilikua na maneno ya ushawishi. Nilikua nina maneno ya kuwakamata walionipa muda kunisikiliza.
Idada ya walionikubali ilinitia kiburi nikajiona hakuna wa kunizingua..
Nikasahau kuwa umri unaenda na mambo yanabadilika. Kila niliyekua naye enzu hizo ameshapata mwenza wa maisha. Wote wameshaanzisha familia. Ule ujana umenitupa. Hata fikra sio kama za zamani.
Kila nikijitahidi kutafuta wa kunielewa na kujitoa kwaajili yangu, sipati tena. Nakutana na wanaohitaji hela na kuhudumiwa kila kitu. Yaani mahusiano yetu ndio yawe yana provide kila kitu kwao.
Maneno matamu yameniisha kinywani mwangu. Yale majivuno sina tena. Kila nikiangalia nilipotoka, najiona nimepoteza sana. Najiona nastahili kupitia haya.
Hivi sasa nipo mwenyewe na mpweke. Sina wa kupiga naye story, sina wa kutokaa naye. Sina wa kuchat naye, sina wa kubebishana naye, sina wa kunijulia hali, sina wa kuniuliza nimeamkaje, sina wa kutaka kujua nimekula au sijala, sina wa kutaka kuja japo kunioshea vyombo.
Yaani kwa ufupi nimepoteza kila kitu...
Nimemaliza