Alone and lonely

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
5,915
Reaction score
7,210
Naweza nikajiita loser. Niliutumia ujana wangu vibaya sana. Nilijiona mimi ndio mimi. Sikutaka kuwa na mahusiano ya kudumu. Nilipenda kupita bila kujali hisia za wale ninaowahitaji.

Nilijiona mimi bora kuliko wengine. Nikawadharau waliojitoa kwaajili yangu. Hakika nilijua kuchezea mioyo ya wanawake.

Japo sina mvuto, hela wala sikutokea kwenye familia ya kitajiri, lakini nilikua na maneno ya ushawishi. Nilikua nina maneno ya kuwakamata walionipa muda kunisikiliza.

Idada ya walionikubali ilinitia kiburi nikajiona hakuna wa kunizingua..

Nikasahau kuwa umri unaenda na mambo yanabadilika. Kila niliyekua naye enzu hizo ameshapata mwenza wa maisha. Wote wameshaanzisha familia. Ule ujana umenitupa. Hata fikra sio kama za zamani.

Kila nikijitahidi kutafuta wa kunielewa na kujitoa kwaajili yangu, sipati tena. Nakutana na wanaohitaji hela na kuhudumiwa kila kitu. Yaani mahusiano yetu ndio yawe yana provide kila kitu kwao.

Maneno matamu yameniisha kinywani mwangu. Yale majivuno sina tena. Kila nikiangalia nilipotoka, najiona nimepoteza sana. Najiona nastahili kupitia haya.

Hivi sasa nipo mwenyewe na mpweke. Sina wa kupiga naye story, sina wa kutokaa naye. Sina wa kuchat naye, sina wa kubebishana naye, sina wa kunijulia hali, sina wa kuniuliza nimeamkaje, sina wa kutaka kujua nimekula au sijala, sina wa kutaka kuja japo kunioshea vyombo.
Yaani kwa ufupi nimepoteza kila kitu...

Nimemaliza
 
Karibu jamiiforums ,bado una thamani
 
Pesa itatatua changamoto nyingi sana ulizozitaja l, kama sio zote. TAFUTA PESA!
Kutafuta kuna kukosa na kupata. Raha upate wa kukufariji pale unapokosa. Hao waliionyesha kunifariji niliwazingua nikajiona mimi ndio mimi. Saizi nakutana na ambao ukikosa, anatafuta mwingine faster
 
Umeshindaje braza? nusuhela I hope you had a wonderful day, na dinner umeipata kwa wakati.

Sasa ni saa za kulala. Usiku mwema na njozi njema ... Malaika wa Mungu wakulinde nyakati zote.
Nimekupunguzia upweke kidunchu si ndiyo?
 
Wewe tu hujaamua,,, mbona kuna wanaume wanaopoa mabinti hata miaka 70?
Inawezekana ila najiona nimechelewa. Siwezi kupata wangu nitaishia kutembea na wapenzi wa watu. Shida ni kwamba wakati wa kufanya hayo umepita natamani ningekua na wangu mmoja tu ambae tungekua tunakumbushana mbali tulikotoka
 
Umeshindaje braza? nusuhela I hope you had a wonderful day, na dinner umeipata kwa wakati.

Sasa ni saa za kulala. Usiku mwema na njozi njema ... Malaika wa Mungu wakulinde nyakati zote.

Nimekupunguzia upweke kidunchu si ndiyo?
[emoji23][emoji23][emoji23]umetisha mkuu
 
Utakuwa na uchu wa mbunye "nyege"
.
.
.
Natania kaka mkubwa!
 
Umeshindaje braza? nusuhela I hope you had a wonderful day, na dinner umeipata kwa wakati.

Sasa ni saa za kulala. Usiku mwema na njozi njema ... Malaika wa Mungu wakulinde nyakati zote.

Nimekupunguzia upweke kidunchu si ndiyo?
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Unazingua
 
Inawezekana ila najiona nimechelewa. Siwezi kupata wangu nitaishia kutembea na wapenzi wa watu. Shida ni kwamba wakati wa kufanya hayo umepita natamani ningekua na wangu mmoja tu ambae tungekua tunakumbushana mbali tulikotoka
Mkuu toka huko kwenye ku feel guilty,,, ruhusu kupenda na kupendwa tena,, some people find love at 60's,,, it doesn't matter how your story has been,,,,,you can still find that special someone,,,be happy and confident with yourself and actively search for that special someone
 
Inawezekana ila najiona nimechelewa. Siwezi kupata wangu nitaishia kutembea na wapenzi wa watu. Shida ni kwamba wakati wa kufanya hayo umepita natamani ningekua na wangu mmoja tu ambae tungekua tunakumbushana mbali tulikotoka
Namba inasoma ngapi now? Wachana na wapenzi wa watu. Muombe Mungu akuoneshee wako ni yupi...
 
Vipi bado haumuamini Mungu na haukubali uwepo wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…