mi nadhani lugha yoyote duniani ni lazima ipitie kwenye misukosuko na mara nyingi matokeo yake ni eidha lugha kufa kabisa au kupanuka zaidi, kiswahili ni mchanganyiko wa lugha nyingi (kichina, hindi, english, kireno, arab,jerumani, kibantu nk), ......
Unataka kumfundisha mtu anayetafuta lughamkato ya mitaani iliyotokana na text messaging systems alifubete ya Kiswahili wakati wafuatiliaji wengi wa kiswahili wa kawaida hawaijui?
hapana sina nia ya kumfundisha mtu lugha ( kwanza mimi si mtaalamu wa lugha) ninachoshangazwa ni kule kutojua wapi pa kutumia lugha gani, mara nyingi watu hutumia lughamkato hata mahali ambapo haiwasaidii sana. Kwa kutumia mifano niliyoishaitoa; ukiandika cjui badala ya SIJUI kuna tofauti gani ya wingi wa herufi ukilinganisha na neno sjui? Tatizo ni kuwa wakati mwingine hata watu wanapoandika insha za maana au hata wanapotoa michango yao hapa jamvini hufanya hivyo. Kwa kweli ni muhimu tukumbuke kwamba kama humfahamu mtu kitu kinachomuwakilisha ni uandishi wake. Endapo unaandika kama Chukulubu basi watu wanaosoma watakuona kama Chukulubu (Chukulubu ni mmoja wa wahusika wa vikaragosi vya chakubanga kama vilivyokuwa vinatokea katika gazeti la Uhuru)

Kwa hiyo unachobonda ni kwamba wanaandika cjui badala ya sjui au kwamba wanakatisha maneno?