mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 901
- 1,742
NIPO SALAMA ndugu zangu Baada ya TUKIO la KUWATOROKA Waliojiita POLISI, Pale Landmark Hotel, Ubungo, Dar es salaam. "Kama Magaidi Wanakamatwa kwa namna ile, Nadhani kuna shida kubwa kwa Vyombo Vyetu Vya dola. NITAELEZA kwa kina but in brief
Nikiwa na Kikao Kazi Landmark Hotel,Ubungo,Walikuja Watu Waliojitambulisha ni Polisi kutoka Makao Makuu, Wakiuliza nani anakisimu kidogo hapa, Tukawashangaa na kuwauliza nini akina nani? WAKADAI Wapo kazini Wao ni Polisi na kutuonyesha Vitambulisho haraka
Wakatuambia hapa Kuna GAIDI Kati yenu tunanamtafuta hapa, MWENYE simu ndogo atoe haraka, Mara kiongozi wa Msafara akapokea simu ya maelekezo Kwamba wote tupo under target. Tukaambiwa tupo Chini ya Ulinzi tangia sasa.
Wenzangu walipoanza kupiga simu kwa ndugu wakapokonywa haraka na kukatokea mzozo Mkubwa baina yetu na Wao, Nikafanikiwa KUWATOROKA kwa njia ya Makuti iliyopo kwenye Mtalo wa Maji na kuibukia Ubungo Darajani na kwenda sehemu salama kwangu
Nimearifiwa na Wakili Wangu, Kwamba Wenzangu Wawili (2) waliowekwa Chini ya Ulinzi na Walipelekwa Kituo cha Polisi chang'ombe na baada ya Mahojiano, Wameachiwa huru kwa hoja Kwamba Polisi Walikosea Target ya MAGAIDI
Hili si tukio la kwanza dhidi yangu, SIWEZI Nikapuuza hata kidogo dhamira yao, Nilipofukuzwa chuo, Nilivamiwa na Watu wa AINA HII na Wakajitambulisha kwa Staili hii hii, Bila WATU DDC, Dar es salaam, huenda ingekuwa HISTORIA
Nimeokoka kwenye tukio hili, sijui la kesho, Nasisitiza kwamba, MAGAIDI Hawawezi kukamatwa kwa namna ile, Najua tunachukua tafadhari kama Binadamu, Namwachia MUNGU Usalama Wangu tangu sassa.