Ama hakika Simba Sports Club ya Msimu wa 2020 / 2021 itakuwa ni ile ya Tema Mate Kushoto kisha Unafukia Kulia na Raha tupu tu!

Acheni ujinga watanzania!
Kwa nini mnapenda kuita watu wazee kisa wamecheza muda mtefu?

Nyie mlipomsajili ngasa mliona ni mtoto?Au kwa vile hana ndevu?
bado manataka kuendelea kusajili mababu??? hivi hamuweze kutengeneza team yenu nyie kwa faida ya miaka 5 mbele!

yaani mnamuota OKWI, pia MORISSON duu
 
Umemsahau Kibubu na babu Kagere, mafanikio ya MO yatakuwa ni kuhakikisha hakuna nafasi iliyo wazi katika baraza la wazee.
 
Hopeless wewe hapo unayemfananisha mnywa ulanzi na buffon (world class)[emoji1787]
Mkuu tofauti nyingine angalia nafasi wanazocheza, Okwi ni mshambuliaji wakati Buffon ni golikipa. Magolikipa huwa hawa kazi ya kukimbia kimbia uwanjani tofauti na wachezaji wengine, ndio maana golikipa kucheza akiwa na miaka 40 siyo hoja. Hivi Pepe Reina na Buffon nani mkongwe zaidi?
 
Nitawashangaa sana viongozi wa Simba kama watamsajili Morison hata kama watampata bure. Ni "bonge la mchezaji" lakini ana nidhamu mbaya uwanjani na nje ya uwanja. Na hata vilabu alivyotoka kabla ya kuja Yanga ana rekodi mbovu za nidhamu. Huyo Morison abakie tu huko Yanga na nidhamu zake mbovu kwani huko anafanya anachotaka wakati wowote na bado viongozi na kocha wanambembeleza utafikiri anaweza cheza peke yake uwanjani dhidi ya timu pinzani. Yaani mchezaji yupo juu ya kocha na viongozi. Hii ni dharau kubwa sana kwa wachezaji wengine wa Yanga wanaoipigania nembo za Yanga na GSM usiku na mchana wakati mwingine bila kulipwa mshahara na hata pesa za usajili kwa wakati.

Kwa timu kama Simba ambayo imeweza kujenga umoja kati ya wachezaji wake wote na kuwa kama familia moja isijiingize katika jaribio la kuleta mtu ambaye atakuja kuleta mgawanyiko kati ya viongozi na viongozi na kati ya wachezaji na wachezaji. Kwa wale wasiofahamu wajue kuwa mafanikio ya Simba kwa miaka hii miwili/mitatu iliyopita yamechangiwa sana na umoja na usawa kwa wachezaji achilia mbali nguzo kuu ambayo ni nidhamu za wachezaji mmoja moja na timu nzima kwa ujumla. Sasa katika hali kama hii ukimleta Morison japo ni mchezaji mzuri lakini utakuwa unavuruga umoja uliojengwa kwa takribani miaka mitatu sasa baina ya wachezaji.

Morison ni aina ya wachezaji matapeli na kumdhibiti ni kumvunjia mkataba kitu ambacho kikitokea anafaidika yeye kama mchezaji. Na ukiendelea kukaa naye anashusha morali ya timu nzima. Na hata anachowafanyia Yanga sasa hivi vituko vyote lengo lake Yanga wachukie wamvunjie mkataba ili aende akasaini sehemu nyingine avute mpunga.

Morison kwa Simba ni "big no". Nidhamu kwanza halafu kipaji ndio kifuate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…