Sijaona uzungu wowote hapo!!!!
Ninachojua, wanaume wana moyo mpana kwenye suala la watoto wa kufikia (walio kuja na Mwanamke)
Mwanamme kama hamtaki mtoto husema waziwazi kabda ya mahusiano kufikia mbali na akikubali huwa harudi tena nyuma.
Tatizo linakuwa tu pale mwanamke anapoficha kuwa anamtoto na kuja kusema wakati wamesha amua kuishi pamoja...
Huo sio uzungu, ndivyo wanaume wa ukweli walivyo...
Kuna wazungu wengi tu ambao hawapatani na watoto/ wazazi wao wa kufikia.
Kudhani hivyo ni ujinga tu (hali ya kutokujua au kufahamu jambo au kitu).
Hakuna tofauti na wale ambao hudai eti Wazungu sijui wana mapenzi ya kweli (ilhali wanatalikiana utadhani wanagaiana njugu) na mara sijui Wazungu hawachepuki.
Ni uongo ulio na msingi katika ujinga kwani mtu yeyote ambaye keshawahi kuishi na Wazungu atajua kwamba hao watu nao ni kama sisi tu....kuna wambea, wapo wasabasi, mahasidi, wenye inda, wachepukaji, makatili, na kadhalika.
Na mtu ukiendelea kuishi na watu wa aina mbalimbali utagundua kwamba wote sisi kama binadamu huwa tunachangia baadhi ya tabia ambazo ni za kibinadamu.
Hivyo, alichokifanya huyo Diamond si kitendo cha Kizungu. Ni cha kistaarabu na kiungwana tu.
Kuna Wazungu wengi tu ambao hawawapendi ndugu zao wa kufikia. Sasa ina maana hao siyo Wazungu au sijui niseme hawana mambo ya Kizungu?
Ujinga uliokithiri bado ni janga kubwa sana.