Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Miujiza ya Allah ni mingi sana.Moja wapo ni katika huu mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ameujaalia uwe ni ujumbe kwa kila binadamu aliye hai.Si kwa waislamu peke yao ila ni kwa watu wa dini zote.
Tangu siku ya mwanzo mwezi unapoanza masoko hujaa wanunuzi.Tulidhani kwa vile watu wanafunga basi kula kutapungua kumbe ndio huongezeka zaidi.Wafanyabiashara wa masokoni wa dini zote hufurahia sana kuingia kwa mwezi huu.
Ikifika muda wa jioni barabara zote huwa na msongamano mkubwa wa waendao kwa miguu na vyombo vya moto kila mmoja akitembea kwa ukakamavu mkubwa.Tulidhani kwa kufunga na kutokula mcha mzima wala kunywa hivyo watu wamekuwa ni dhaifu.Kumbe watu ndio wamezidi kuwa wakakamavu.
Habari kubwa iko kwenye maduka ya nguo.Wafanyabiashara wote wanajitayarisha vya kutosha kupata mauzo ambayo huenda ndio makubwa katika mwaka mzima,
Nani asiyeujua mwezi mtukufu wa Ramadhani.Siku watakapohojiwa kwanini hawakufungua lipi litakuwa jibu lao.