KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Tumekamata mwizi tukaanza kukung'unta, piga mwizi mpaka akapandisha mapepo!. tukajua anatania tukaendelea kupiga tu! wacha mapepo ya mwizi yacharuke zaidi!, yakagoma hayasikii chochote ukirusha jiwe linadakwa linarudishwa!.
mshale unakwepwa tukaona hii ishakuwa serious mapepo yakawa yanaongea kiarabu mixer kibantu cha kizuru!.
wengine wakaanza kukimbia kuona mwizi ameamua kubadili miondoko!, wenye mioyo migumu tukamvizia tukamkaba shika miguu, shika mikono akaturusha! alikuwa ananguvu kama ngiri!.
wengine waliokuwa na macho makali wakausoma mchezo wakaona hii ngoma nzito wakakimbia!.
tukabaki mtu tano tunaojiamini sasa!, tukasema huyu tunamalizana nae kiroho maana kimwili tushamshindwa!.
tukamkaba tena shika mikono na miguu! plan ni kumuombea kwanza madude yake yashuke halafu ndo tumalizanenae kimwili! kumbe password moja tulikuwa tumesahau ya kwamba ktk hao tuliopo hakuna mtu wakiroho!..
achana tu na kwamba hayupo huyo mtu wakiroho bali ktk harakati za kumshika wale wenzangu wanne wakawa wamemgawana vyema yani wameenea wamembana mikono na miguu vilivyo!, hivyo mimi ndo nikawa nipo huru na maana ya huo uhuru tafsiri yake mimi ndo natakiwa nimshike kichwa halafu nishushe maombi!!!!..
kwa jinsi navyojijua ni kasongo nikajiseti kwanza nikajiangalia ndo nagundua nipo kifua wazi, nimevaa pensi na mguuni nina rapa moja na hilo rapa lenyewe limenipanda mguuni mkabala na goti!.. wenzangu kuona nachelewa wakaanza kunipigia kelele!
nikawambia watulie hapohapo chapchap nikaweka mikono yangu yote miwili kwenye kichwa cha yule mwizi japo kilikuwa hakitulii!, nikafumba macho nikazama kiroho nikaanza.
fire fire fireeeeeeeeee!
toka pepo, pepo toka sasa ile nataka kusema tu lile jina la kumaliza shughuli yule mnazareti ndo mambo yakaharibika!.. nilisikia "puuuuu" hahaha!.
Hapo hakukuwa na kuuliza nini kimejiri, hili balaa lilikuwa halinunuliki kwa bei yoyote ile!, isitoshe ilikuwa ni usiku njia ni kukimbia unachosikia kinachokufuata nyuma wala sio kufuata uelekeo fulani!.
Hakuna aliebaki yale maombi yakumuombea yule mwizi ya kwamba pepo toka naona sisi mtu tano ndo tulikuwa hayo mapepo maana sio kwa kuondoka kule!!! vilikuwa vinasikika vishindo na mihemo tu!.
mbaya mbovu mwizi aliunga na mimi!, yani pepo wake wabaya waliona mimi ndo tabu ya yote yaliyompata kiti wao!, wakati kaka wa watu nilikuwa sijui hata mwizi huyu kaiba nini!!.. na hapo ndipo nilipokumbuka ule usemi wa "kusikia kwa kenge mpaka....."
maana nilishagaonywa kutoingilia mambo yasiyonihusu lkn mimi kaka wa watu huwa sikomi!.
Nilikuwa nakimbia huku napiga kelele lkn nani aje aungane kwenye mbio hizi za binadamu aliepagawa na mapepo akimkimbiza kenge asiesikia!..
Bahati nzuri yule mwizi alikuwa anamajeraha hivyo hakuweza kumudu kukimbia sana, isipokuwa tu yaonyesha alikuwa ananguvu sana maana vishindo vyake vilikuwa kama vya ng'ombe!.
hiyo ndo ikawa ponapona ya kenge ambae kusikia mpk atoke damu!.
kulipokucha naambiwa yule jamaa kumbe alikuwa hajaiba!, alifumaniwa huko mtaa wapili sasa aliemfumania alipoanza kumkimbiza akaamua apige mwano wa mwizi kumbe ni mgoni!.. mi nafikiri jamii ilete mwano wa ugoni ili msituchanganye mtakuja kutuua bure watu wengine wanatembea na vitu vizito kichwani mwao!.