Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Ile kauli ya 'anaupiga mwingi' inaweza kuwa na ukweli kuliko tunavyodhani. Yaani ni mchakamchaka wa kufa mtu.
Ikitokea tu kuna mjadala wa moto unaendelea basi ndani ya siku mbili tatu unakua umezimwa kwa matukio mengine ya moto zaidi
Mara hawa wanadai Katiba Mpya huku Sabaya anakamatwa, kule bei ya mafuta inapanda, huku Diallo anamsimanga mwendazake, mara sijui tozo za miamala zimepanda, sijui wagonjwa wa corona wako kwenye oxygen, haujakaa sawa soko Kariakoo limeungua, sijui nani huko katuma picha zake za uchi. Ni matukio mfululizo, full throttle.
Vichwa vya wadanganyika viko fully occupied 24/7. Choir master anaonekana anaimudu kweli kazi yake. Miluzi kila kona yaani mbwa kachanganyikiwa kabisaaa.
CHADEMA msipokuwa makini mtakuwa mnadandia hoja mpya na kujadili matukio kila siku, maana ma producer wa matukio wanafanya kazi overtime.