Amaan Stadium ni mbovu, kama kuna upigaji watu wawajibishwe

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
Kumekuwa na hali ya kuupamba sana huu uwanja uliofanyiwa ukarabati wa Amaan Stadium hapa Zanzibar, kwakweli bila kupepesa macho wameshindwa kwenda na mabadiliko na maendeleo ya sasa katika sekta ya michezo Duniani.

1. Eneo la kuchezea (pitch) haliendani kabisa na zile mbwembwe tulizoziona, quality ni ndogo kwakweli.

2. Taa bado ni tatizo,nikajua zitakuwa kama zile zilizofungwa MKAPA STADIUM angalau zikaribie basi,..yaani taa kama za KAITABA unaona vivuli vinne vinne.

SMZ kwa hapa mmechemka ,kama kuna upigaji chukueni hatua ila kama ndio halali yake vile basi JIPANGENI TENA.


 

Attachments

  • mickyjnrofficial-20231228-0001.jpg
    100.8 KB · Views: 4
Binadamu hamna jema kabisa. Jifunzeni kukubali vitu vizuri hata kama roho zenu zitawauma.

Hizo ni changamoto ndogondogo ilitakiwa uwaitishe wahusika wazishughulikie. Sio kila kitu ni upigaji mkuu.
 
Kosa jingine ni kuweka nyasi bandia ( artificial turf) ambazo kwa Sasa si chaguo katika soka.

Nyasi bandia huchochea majeraha ya vifundo kwa wachezaji, pia nyasi bandia hazifai kucheza wakati wa Jua Kali.

All in all wamejitahidi[emoji123]
 
Binadamu hamna jema kabisa. Jifunzeni kukubali vitu vizuri hata kama roho zenu zitawauma.

Hizo ni changamoto ndogondogo ilitakiwa uwaitishe wahusika wazishughulikie. Sio kila kitu ni upigaji mkuu.
Hela mmezifanyia nini? Uwanja una taa kama za Xmas 🎄 tree
 
Kitu ambacho na Mimi kimenitia shaka ni gharama za ukarabati ukarabati kufikia billion 56 kama nilimsikia vizuri mtangazaji.
Mbaya zaidi kiwanja kufanywa kuwa Cha nyasi bandia uku kapet lake ambalo ni jipya Kuna namna mchezaji akipiga mpira au ajikwaa linatoka vumbi.
Kuna tofauti kwenye macho Yangu kama mtazamaji nikiangalia uwanja wa Azam complex na uu wa Amani ambao umekarabatiwa sehemu ya kuchezea.

Kwa ninavyo uona uwanja wa Amani kilicho ongezeka ni paa kuzunguka uwanja mzima , Nyasi bandia na viti ambavyo vipo majukwaaa yote.
Ila sijajua kama vile viwanja vya nje ya Amani vimekarabatiwa na kwa kiwango Gani.
 
Binadamu hamna jema kabisa. Jifunzeni kukubali vitu vizuri hata kama roho zenu zitawauma.

Hizo ni changamoto ndogondogo ilitakiwa uwaitishe wahusika wazishughulikie. Sio kila kitu ni upigaji mkuu.
Nyeusi ni NYEUSI,na nyeupe ni NYEUPE....hatuna muda wa kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa,zama za nyasi bandia tumezipita.....
Zanzibar ni mji vutivu sana ulipaswa kuwa na viwanja vikali zaidi ya kile cha mkapa kama viwili au vitatu.....siku moja unaona Arsenal wanaweka kambi ya pre season visiwani sio kutuwekea minyasi bandia ambayo kila siku wanaipiga vita
 
Kingine cha kushangaza, eti viwanja vya mazoezi pembezoni mwa uwanja wa Amaan navyo vinaenda kuzinduliwa. Yaani timu zilizowahi kufika Zanzibar havijapewa nafasi ya kuvitumia mpaka Yanga na Simba waanze wao kuvitumia. Hawa watu wangeachwa mpaka kwanza waonyeshe wako serious
 
Kama uliangalia simba vs wydad hazikuwepo wameweka yale ma bati yalibandiwa stika.
Nmeenda YouTube kuangalia tena highlights za mechi ya Simba SC vs wydad ac.
Hizo screen za Matangazo ya digital zilikuwepo, hayo yasiyojongea yaliwekwa mbele ya hizo screen.

Zipo kabisa, chunguza vizuri kabla ya lawama boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…