Kwa taarifa nilizo nazo za uhakika, Benki hii makao makuu yake yako PPF Tower 3rd Floor kwa muda na mwezi March,2012 itahamia jengo la jirani PSPF 1st floor. imeanza na branch moja kariako na baadae January itafungua Nyerere Road karibu na Quality Plaza na march PSPF chini. Unaweza kwenda kufungua account moja kwa moja Kariakoo au Makao makuu.
Jinsi inavyofanya kazi, ni benki kwa ajili ya wote, ni benki inayofuata Sharia Priciples, tofauti kubwa na benki zingine ni kutokutoza riba na inashughulika na biashara halali (ina maana kampuni kama TCC, Breaweries, nazinginezo kama hizo hazitapata nafasi kwenye benki hii) Tofauti naainisha kama ifuatavyo
Deposits
Depositors (Fixed deposit & Savings) hawatalipwa interest, bali watashare na benki mapato yatokanayo na kufinance miradi mbalimbali kwa uwiano utakokubaliana mwanzo kama 70% kwa 30% etc.
Mikopo
Mteja ataleta proposal ya chochote anachotaka kufanya ila kiwe halali, then bank inatanunua na kumuzia kwa faida, kwa mfano wataka gari toka Japani, utapeleka profoma invoice bank na benki itanunua gari hilo likishafika bandarini na kukombolewa utauziwa kwa faida na kuanza lipa benki kwa instalment,kama nyumba benki italipa contractors, kama hardware, benki italipa unako agiza nk nk, cha muhimu hapa hupewi cash, (maana wanaopewa cash wanafanyia biashara tofauti na walivoombea,matokeo kudefault.