Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Amani Golugwa amesema msimamo wa chama hicho kutosaini kanuni za uchaguzi Mkuu 2025, wanajiona wako sawa huku akikisisitiza hawatakimbilia kusaini zaidi ya kufichua yasiyofaa.
“Tunaona tunaenda sawa kabisa na watu wanazungumza operesheni yetu ya ‘No reforms, no election’ hivyo mkakati huu tunaenda nao sawa kabisa,” amesema.
GOlugwa ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 16,2025 wakati akichangia mjadala wa Mwananchi X Space wenye mada isemayo: Kanuni za maadili ya uchaguzi 2025 na mustakabali wa siasa za Chadema ulioandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL).
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Msingi wa hoja yake ni kwamba, kusainiwa kwa kanuni hiyo ni takwa la kifungu cha 162 cha Sheria ya Uchaguzi wa Marais, Wabunge na Madiwani, kinachovitaka vyama vya siasa, Serikali na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kusaini kanuni hizo.
Aprili 12, 2025 Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Ramadhan Kailima alisema Chadema hakitashiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba na chaguzi ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano baada ya chama hicho kususia kusaini kanuni, hivyo kukosa sifa ya kushiriki mchakato huo.
“Hili la kanuni hatutafuti kuridhiana hapa, hapa tunatafuta mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi, hatutakimbilia kusaini kanuni isipokuwa tutaendelea kuyasema yanayotakiwa kufanyiwa mabadiliko,” amesema Golugwa.
Amesema kanuni hizo zinatumika kama fimbo ya kuvichapia vyama vya upinzani.