Amani Karume: Nilishangaa wana-CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, Uchaguzi 2015 Zanzibar nilisikitika, niliwauliza hawa wenzetu si Watanzania?

CCM ni walewale sema tu ameamua kuzuga
 
Sijui kwanini wakishastaafu ndio akili huwarudia?

Au pia huwa wanatuchezea makusudi wakijua muda wao wa kutubu utafika na watafanya hivyo, kwa mtindo huu naona hata hawa wa sasa nao siku inakuja watatubu.
Wanajua hatuna akili
 
Mungu akuongezee umri na afya tele.....wachache sana tena wqlioonja keki ya Taifa ukiweza kusema ukweli wa moyo....blessed Baba na mwana mko fikra huru
 
Mbali ya kutosema hadharani tokea wakati huo juu ya dhulma hiyo, je alichukuwa hatua gani kama mmoja wa viongozi ndani ya chama chake ambacho kilifanya dhulma ya aina hiyo? Je ameendelea kuwa kwenye nafasi yake ndani ya chama ama alijiweka pembeni kupinga kwa vitendo juu ya dhulma hiyo? Je aliye dhulumiwa alikuwa ni maalim seif ama ni wananchi wa zanzibar akiwemo na yeye mzee karume?
 
Shetani akizeeka anageuka kuwa malaika
 
Haya maneno huwa wanayasema baada ya kustaafu, siwaamini, yale yale ya Mkapa kitaka Katiba Mpya kwenye kitabu chake baada ya kustaafu.

Hata Karume binafsi asingekubali kushindwa na Seif na angetumia njia yoyote kuhakikisha anashinda.
Mbona yeye 2005 alishindwa na Self na hakuachia?
 
Walao kikubwa ameyasema akiwa yeye binafsi bado yupo hai na CCM kama taasisi inayolea huo uharamu bado ipo madarakani,amechelewa lakini ametimiza wajibu wake wa kuweka wazi na umma umemsikia
 
Angekemea kipindi kile cha 2015,kwasasa namuona ni walewale ccm
 
Haya maneno huwa wanayasema baada ya kustaafu, siwaamini, yale yale ya Mkapa kitaka Katiba Mpya kwenye kitabu chake baada ya kustaafu.

Hata Karume binafsi asingekubali kushindwa na Seif na angetumia njia yoyote kuhakikisha anashinda.
Kuna maneno kutoka vijiwe vya gahawa kuwa kuna mmoja Kati ya sheni au karume alikubali matokeo ya kushinda kwa sababu alisema kudhulumu matokeo kwa mujibu wa dini yake ni dhambi,na yeye haitaki dhambi hiyo.
Nasikia Mkapa na konvoi lake wakatua visiwani kwenda kumchana live,
Baada ya kichano hicho akatanganzwa kuwa mshindi.
Vijiwe vya gahawa bana!
 
Na akaendelea kutawala kwa raha zote miaka 5, leo katoka ndo anasononeka
Huyu mbona alimaliza Urais wake kabla ya 2015, wakati huo Rais alikuwa Dr Shein ambaye ndiye baada ya kufutwa kwa matokeo na uchaguzi kurudiwa alishinda awamu ya pili na kuendelea kuongoza.
 
Huyu mbona alimaliza Urais wake kabla ya 2015, wakati huo Rais alikuwa Dr Shein ambaye ndiye baada ya kufutwa kwa matokeo na uchaguzi kurudiwa alishinda awamu ya pili na kuendelea kuongoza.
Nilisha sahau kama jecha S. Jecha ilikuwa kwa shein nae hakutaka kulikemea hilo
 
Amani aka HAPA PANGU ni mnafik mkubwa! Hata awamu zote alizogombea yeye Maalim seif alisema ameshinda uchaguzi je ilikuwa kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…