PostGE2025 Amani kwanza, haki baadae ni Msingi wa dini mpya ya wasiojulikana?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam!

Ni kama kuna dini na Imani mpya imeingia nchi ni,

Kikundi na itikadi hii ya Siri imeingia kwa viongozi mbalimbali wa dini, wasanii, wanasiasa, polisi,waovu Katika makundi mbalimbali wakijaribu kuuaminisha umma wa watanzania kwamba AMANI ndio Msingi wa HAKI.

Msemo huu unaoenezwa kwa Gharama kubwa unakwenda tofauti kabisa na vitabu vya Imani vyote visemavyo HAKI ndio mama wa AMANI. Kwa muktadha huo, Msingi wa dini hii mpya ya gizani, ni kupingana na neno la Mungu ambalo linasema Haki inatangulia kabla ya Amani.

Muasisi wa Taifa hili Mwl Nyerere Katika hotuba zake mbalimbali ambazo kwa sasa ziko kapuni kwa malengo maalum, amekuwa akisisitiza kuwa Haki ni Msingi wa AMANI, akihimiza vijana wa Taifa "KUASI" mifumo kandamizi inayodidimiza haki za wananchi.

Yaani maana ya kudai AMANI kwanza haki baadae Katika msingi wa dini hii mpya ni sawa na kusema;

1. Tunatangaza mshindi fake, Katika uchaguzi batili, fake Ulioyeyuka, Kisha tunaomba maridhiano ,angalizo likiwa, Tunza Amani ndipo haki itakujia🤔

2. Risasi za moto zinatumika kuua raia wasio na silaha, Kisha waliohusika kuua wasiguswe, Kisha ndugu za marehemu wanakumbishwa kuwa kaa kimya, usidai Haki, Bali tunza AMANI ndipo haki itakujia baadae.

3. Wananchi toeni maoni juu ya katiba mpya muitakayo, Maoni hayo ya wananchi kupitia Tume ya judge Warioba yanawekwa kando, kinatengezwa kitu kingine ,kamati fake ya kukusanya maoni fake, Kisha ilete mapendekezo fake ya kuwakinga viongozi batili Kisha wananchi wanakumbishwa kuwa Tunza AMANI, madai ya katiba hatushinikizwi na yeyote kuyatekeleza, Tunza AMANI,,haki baadae.

Swali: Hii dini mpya ya gizani itafanikiwa?

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿.

Nawasilisha
 
Ukiwaulliza,

Neno AMANI kwanza ,HAKI baadae, imeandikwa kifungu kipi ndani ya BIBLE au Kitabu Cha Islams?

Utajibiwa,

Rudi kwenye kiitikio kwamba,

Tunza AMANI kwanza, HAKI baadae.

Tutafika?
 
Amani na haki ni pande mbili za shilingi.
"There can be no peace without justice, and no justice without peace.” — Pope John Paul II
 
DINI YA MAKAFIRI YA WAISIHARAMU
 
 
Your browser is not able to display this video.

Amani ni Matokeo/matunda ya palipo na Usawa, Haki, Upendo n.k
Kwa hali kama hii👆🏾 (video) tumeshatia doa kwenye msingi, Amani itapatikanaje? Ikiwepo basi ni fake, ya maigizo... ya ku-mask tu hasira, huzuni, chuki, uchungu vivilivyopo ndani.
 
Yani kama ulikuwa kwenye mawazo yangu ukaandika huu uzi.

Yani amani taifa hili inatafsiriwa tofauti sana

Maana ya wao amani ni wafanye wanavyotaka ikiwemo kuua, kuteka, kuiba rasilimali, ufisadi, uchaguzi usio huru na haki n.k lakini wananchi mkae kimya msidai chochkte ndo maana ya amani kwao.

Kwamba mtu akisimamia ukweli kwa kupinga rushwa, udisadi, sheria kandamizi, utekaji, kuua wananchi na kudai katiba iliyo bora wao kwa tafsiri yao ni kuleta uvunjifu wa amani.

Niseme hatupo serious kama nchi tunakoelekea sio kwa kiburi cha wanaojiita watawala wetu.
 
Mimi nadhani Gen Z waanzie tu pale walipoishia, ili ukombozi wa kweli upatikane kwenye hili Taifa lililotekwa na wahuni.
 
Kwao kudai haki ni kuvunja AMANI.

October 29,

Hapakufanyika uchaguzi,

Uchaguzi batili, fake Uliyeyuka.

Sisi tunadai HAKI yetu ya kikatiba ya kupiga kura Katika Sanduku halisilonajisiwa baada ya kupatikana katiba mpya na tume huru ya uchaguzi,kwamba kudai huko HAKI ni uasi na uhaini.

Hili halikubaliki.
 
Sahihi haikubaliki hata kidogo
 

Sasa tumfuate YESU au PhD?? 🤣

MSIKIE YESU 👇

Yohana 20:21
“Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.”

AMANI KWANZA 👇

Luka 10:5
“Na nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwe nyumbani humu.”

1 Wafalme 5:4
“Ila leo Bwana, Mungu wangu, amenipa amani kila upande; hakuna adui, wala tukio baya.”
 
YESU awambia wanadunzi wake:

Haki yenu isipozidi haki ya mafarisayo, hamtauingia uzima wa milele

Karibu.
 
Ukiwaulliza,

Neno AMANI kwanza ,HAKI baadae, imeandikwa kifungu kipi ndani ya BIBLE au Kitabu Cha Islams?

Utajibiwa,

Rudi kwenye kiitikio kwamba,

Tunza AMANI kwanza, HAKI baadae.

Tutafika?
Ndio tutafika maana maisha ni safari na akuna safari isiyo na mwisho hapa duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…