SueIsmael
JF-Expert Member
- Dec 11, 2013
- 932
- 1,282
Wakuu,
Kwa muda mrefu tumekuwa tukitumia hii misamiati katika maisha yetu: "amani na usalama". Hata hivyo ni dhahiri kuwa jinsi tunavyofafanua misamiati hii katika maisha yetu ya kila siku, kunaweza kuwa na utofauti. Tunaposema kuwa tunaitakia nchi yetu amani na usalama, je tunamaanisha kutokuwepo kwa vita? Je hii ni maana tosha ya kuwapo na amani na usalama nchini? Labda, hiyo ndio maana pekee tutakayokubaliana nayo au labda kuna maana zaidi ya hiyo.
Kwakuwa jamvi hili linajumuisha watanzania kutoka makundi mbalimbali ya jamii yetu, hebu tujadili hapa kwa kujibu maswali haya mawili:
1. Katika maisha yako, ni nini kinakupa amani? Au viashiria vipi katika maisha yako lazima viwepo ili uwe na amani?
2. Usalama una maana gani kwako? Au ni viashiria vipi lazima viwepo ili ujihisi salama?
Nawasilisha