Uchaguzi 2020 Amani ya nchi hii ipo mikononi mwa wakurugezi pamoja na Tume ya uchaguzi

Uchaguzi 2020 Amani ya nchi hii ipo mikononi mwa wakurugezi pamoja na Tume ya uchaguzi

Joined
Jun 17, 2020
Posts
75
Reaction score
268
Kilichotokea mkoani Songwe na kupelekea umauti wa Mtanzania ni ishara kwamba amani tunaivuruga wenyewe hasa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia haki wanashindwa kutumia hekima wala busara mahali panapohitaji hekima au busara kwa maslahi yao au itikadi ya chama Fulani.

Ni mambo ya hovyo kumkata mgombea kipindi hiki eti kwa sababu hajakidhi vigezo alafu ambao hawakidhi vigezo ni wapinzani tu. Mimi sijawahi kuona MwanaCCM amekatwa eti sababu hajakidhi vigezo, ni mambo ya ajabu kweli alafu mnawaaminisha watanzania kuwa wapinzani ndo wanaharibu Amani! Tendeni haki muone kama kutatokea vurugu!

Wakurugezi wa tume ya uchaguzi tendeni haki msiwape Polisi kazi nzito sababu ya itikadi zenu! Pale Zazibar wagombea ACT wamekatwa eti sababu hawajakidhi vigezo, mambo ya hovyo sana! Mbona hamna mgombe wa CCM hata mmoja alienguliwa kwa sababu ya kukosa Sifa??? Jueni watanzani sio wajinga kinachofanywa wanatazama na wanafahamu kinachoendelea.

Jana Katambi anasema eti nchi hii haina wapinzani watakaompigia kura Lissu, zile ni ndoto za Mchana, upinzani upo moyoni na wapinzani nchi hii ni wengi kuliko anavyofikiria asidanganye kuwa lowassa au sumaye alihama nao, yy aendelee kutetea ugali wake lakini sio kusema nchi hii haina wapinzani!

Wasimamizi wa uchaguzi tendeni haki msiwaonee wapinzani,na msiwape Polisi kazi nzito!!
 
Songwe kuna nini kimefanywa na hawa wahuni wa kiwango cha kuzimu?
 
Diwani wa chadema kakatwa kapelekea vurugu hatimaye Mtu mmoja kufariki na wengine kujeruhiwa vibaya sana
 
Back
Top Bottom