Simiyu Yetu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 18,949
- 4,639
Amani kwenu wakuu,
Leo na kesho ni siku za mapumziko lakini pia zimeelezwa kama ni siku za kusoma kanuni tulizopewa ili jumatatu mijadala ianze rasmi ya kujadili kanuni hizi na kuzipitisha ili zituongoze kwenye mijadala ya kupata katiba ya watanzania.
kwa mda wote wa siku mbili jana na leo amani miongoni mwa wajumbe inazidi kuwa kubwa na kuendelea kuwa na moyo wa kufanya kazi baada ya swala la posho kuibua mzozo siku za hivi karibuni.
Tangu kuundwa kwa tume ya kufuatilia ufumbuzi wa swala la posho sasa wajumbe wameichia tume tukiamini kuwa busara zitatumika kupata mwafaka ambao kila mjumbe na watanzania kwa ujumla watalizika na huo uamuzi wa tume teule ya kificho.
Naamini kuanzia jumatatu wajumbe wote tutakuwa kitu kimoja kujadili kanuni kwa mlengo wa kitaifa wala si vinginevyo tupinge jitihada zote za kutaka kuvuruga mchakato kwa matakwa ya watu binafsi.
Ndugu wanajf nashukuru sana rais kuniteua kuwa mmoja wa wajumbe wa bunge la katiba sasa nimeweza kuona angi halisi za wanasiasa wengi walivyowanafiki kwa watu hasa wanapokuwa majukwaani make hujigamba kuwa wao ni watetezi wa watu kumbe usiku hewa ni adui wa wanachi namba moja.
Mungu ni mwema katiba itapatikana kwa rehema zake muumba tutashinda na hatimaye watanzania kupata katiba yao.