Amapiano ni Ushamba wa wasanii wetu au fasheni?

Sijawahi kuielewa Amapiano, japokuwa naona kama midundo hii inatrend Africa kuliko midundo ya Kinaija, ila mimi bado mpaka sasa hamna hata nyimbo niliyo ielewa.
Una matatizo wewe tafta ngoma inaitwa Vula Vala uone balaa lake!

Usipoelewa utakuwa mnywa juisi wewe, siku ukianza ulabu utaelewa!
 
Huezi kumkuta King Kiba anaiga huo upuuzi,. Kuna visanii vinapenda kuigaiga kila kitu ili mradi waonekane wametoa kazi

Kila nchi kuna wasanii wanaimba tatizo naloona kwanini naija na amapiano inafanya vizuri sababu kubwa ni ushirikiano pia kuwa na uchumi kuwa mkubwa South Africa na naija waliacha kupiga nyimbo za wasanii kutoka nchi nyingine ili kukuza mziki wao
Sisi hatufanyi hivyo ndio ata wasanii wanashindwa kuwa na msimamamo
 
Huezi kumkuta King Kiba anaiga huo upuuzi,. Kuna visanii vinapenda kuigaiga kila kitu ili mradi waonekane wametoa kazi
Bora unyamaze huyo mnafiki aliyejaa chuki na wivu, wakati Mondi akitumia biti za kinaija kwa baadhi ya nyimbo zake aliponda sana "...mimi naimba bongo fleva ..naiwakilisha bongo fleva.....king of bongo fleva".

Kavumilia kaona isiwe tabu kuanzia DODO, SALUTE na JELOUS zote biti za kinaijeria, bongo fleva kaipiga kapuni na yeye baada kuponda sana wasanii wanaolipia instagram kwa ajili ya kuzitangaza nyimbo zao, juzi nae kaanza kulipia insta kwa ajili ya kupromoti nyimbo zake ya Jelous.

Huyo ni mnafiki husishangae kesho nae akaimba Amapiano.
 
Kama ndo hela ipo hapo kwenye style za amapiano akuna shida,watu wanatazama fursa iko wapi kisha wanaichangamkia.
 
Reactions: Qwy
Azawi ana ngoma inaitwa quinamino naikubali sana
 
Mshana Jr njoo tusikilize Wana Sikinde Ngoma ya ukae hapa barazani kwangu πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…