AMATB - Niulize Chochote Kuhusu Tehama na Biashara

AMATB - Niulize Chochote Kuhusu Tehama na Biashara

Hivi ni namna gani ukijua coding utaweza kupata kazi na kutengeneza Pesa kwa hapa bongo,
Unapata pesa kwa kutatua matatizo yanayoisibu jamii, yale matatizo mchomo kiasi cha mtu au biashara kukubali kukulipa.
Lakini pia unaweza pata pesa kwa kuuza ujuzi na ushauri.
Na ni kwa C++ na Python zinatosha kukupa hizo kazi?
Inatagemeana unataka kufanya nini. Hizi lugha ni kama vifaa vya kazi. Kama plan ni kuchonga mbao basi hakikisha una randa.
Kabla hujachagua ukajifunze lugha ipi, hakikisha unajua unataka kuja kufanya nini!
 
Unaweza kujifunza software engeneering kutoka Alx academy ya south africa ni free ila uwe committed usipofikisha 80% kwenye project wanakutoa
 
Hivi ni namna gani ukijua coding utaweza kupata kazi na kutengeneza Pesa kwa hapa bongo,

Na ni kwa C++ na Python zinatosha kukupa hizo kazi?
Shida kwa vijana wengi ipo hapa.Na mkuu Mtangoo alishaweka hili sawa sawa.Technologia na coding ni nyenzo tuu za kukusaidia kufanya kazi.Ili upate hela unatakiwa uwe MBUNIFU kwenye kutoa suluhisho la matatizo mengi yanayoizunguka jamii kwa kutumia hizo skills utakazozipata.
Na matatizo yako mengi sana yanayohitaji technologia kuyasolve kuanzia sekta ya kilimo,Biashara,michezo n.k
 
Unaweza kujifunza software engeneering kutoka Alx academy ya south africa ni free ila uwe committed usipofikisha 80% kwenye project wanakutoa
Leo nimetumiwa email ya Kuwa mmoja wa watu walio kuwa selected na ALX Africa, software engineering ya 12 month, nimejaribu kupitia mtandaoni naambiwa ni moja ya course ngumu sana kama hauko committed kuisoma.
Wish me Lack
Kufanikisha.
 
Back
Top Bottom