Ambangile: Yanga ni kama vile walishtukizwa kwamba leo kuna mechi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Hii mechi unaanza kuichambulia wapi hasa kwa upande wa Yanga ? Maarifa hakuna , wapo slow sana , hakuna ubunifu , pasi zisizo na ufanisi , ni kama vile walishtukizwa kwamba leo kuna mechi na nafikiri hata Club Africain hawakuamini macho yao jinsi gani wamerahisishiwa mechi

✍🏻Shape yao ile ile 4-2-3-1 , walitaka zaidi kupitia pembeni kwa kutumia kasi ya mawinga wao wote wawili Kisinda na Morisson , lakini kiungo cha Yanga kilikuwa slow sana , Kisinda na Morisson wanataka mpira mguuni badala nyuma ya safu ya ulinzi na hata wakipata mipira inapotea kirahisi

✍🏻Nafikiri Club Africain wamefanya kile ambacho walitakiwa kufanya , hawakuwa na nia kubwa ya kutaka kufunga haraka , bali waliwaachia Yanga mpira na wao kuwa nyuma zaidi ( 4-5-1 na mara nyingine 4-4-1-1 ) ... game plan yao

1: Zuia kwa idadi kubwa ya wachezaji

2: Ukipora mpira katika upande wa Yanga fanya shambulizi la kushtukiza

3; Ukipata mpira katika upande wao , poozesha mchezo kwa pasi fupi fupi na kushinda faulo za kupoteza muda

Na kwa asilimia kubwa walifanikiwa kwa kipindi kirefu cha mchezo wakiamini mechi ya marudiano wakiwa kwao watakuwa hatari zaidi ya walivyocheza leo

✍🏻Nafikiri hii mechi hata useme uichambue kimbinu ni Club Africain ndio wamefanikiwa kimkakati na Yanga wameshindwa kuuliza maswali magumu dhidi ya wapinzani wao

NOTE
1: Mpinzani akipaki Bus na wewe ukicheza slow na ukipoteza pasi kirahisi basi inakuwa kazi rahisi sana kwa mpinzani

2: Timu moja ilikuwa inajua inachofanya uwanjani ( Club Africain ) na timu moja ilikosa maarifa katika nyakati sahihi

3: Dakika 90 zimeisha , bado 90 zingine za Tunisia ... nani atasonga mbele ? 🤔🤔

FT : Yanga SC 0-0 Club Africain

Credit: George Ambangile
 
Yanga hata hatujui tatizo ni nini? Wachezaji wanapewa kila kitu wapumbavu wale alafu wanacheza kama wamelazimishwa.

Kiukweli kocha Nabi amemfikia mwisho wa maarifa yake.
 
Ambagile acha nawew kuleta unyakyusa wako hapa kila kitu unaachambua. Kmchambulie mkeo maharage mbimbi wew
 
Kwa huo utopolo alioandika hapo ni mchambuzi gani atatembea nao?
Jama anajionaga bonge la mwerevu hkn kitu pale washukuru daimond kawapatia kijiwe Cha Kuja kuzuga asbh na jioni

Hata mpira hajawi kugusa dah bongo noma San kila mtu mchambuzi mm huwa siwazikilizi kbsa
 
Halafu wanategemea wapongezwe na Raisi wetu kweli.
Kwa hii aibu ya Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…