Ahmed Saidi
JF-Expert Member
- Oct 15, 2019
- 1,588
- 3,487
Habari wapendwa,
Kwa tafsiri yangu ambayo sio rasmi, uchawi ni jambo ambalo huwezi kulielewa kwa akili ya kawaida lakini binadamu hulifanya jambo hilo na hata mtu anaelifanya huwenda hajui hutokea vipi. Jambo hili la uchawi pia haliwezi kuelezewa kisayansi kwasababu sio jambo linalofuata kanuni za kisayansi.
Binafsi naamini kwamba Kuna uchawi kutokana na kuwepo kwa matukio kadha wa kadha katika maisha ya kila siku. Lakini naona ajabu kabisa kuna watu wanapinga kabisa kuwa hakuna uchawi na watu hao husema hizo ni fix tu na story za vijiweni.
Kwa ambao hawaamini jambo hili, naomba mnipe ufafanuzi wa kisayansi kivipi matukio haya yanawezekana?
1. Kuna tukio la mama kujifungua kuku kule kigoma. Hili tukio ni maarufu sana ambapo Kuna mama alijihisi ni mjamzito na alihudhuria kliniki kwa kipindi cha ujauzito wake lakini ulipofika muda wa kujifungua huyu mama alijifungua kuku. Uzuri wa tukio hili lilithibitishwa na polisi pamoja na daktari na kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari. Sasa je kivipi jambo hili huwezekana katika hali ya kawaida?
Ripoti ya madaktari ilisema kuwa ni mambo ya kishirikina tu.
2. Tukio la pili nililiona mwenyewe Kwa macho yangu. Ilikuwa Niko darasani nafundisha wanafunzi wa kidato cha sita, ghafla mmoja akapandisha kinachoitwa mashetani, hii huwa inawatokea watu wengi sana. Kupandisha mashetani pekee sio uthibitisho kuwa kuna nguvu za Giza lakini hile hali ya mtu mwenye mashetani kuwa na sifa flani ndio inanipa maswali mengi. Watu wengi waliopandisha mashetani huwa na nguvu sana.
Yule mwanafunzi aliepandisha mashetani alikuwa na nguvu kubwa kiasi aliweza kuwazuia takribani watu kumi na kuwabwaga wote na akafanikiwa kukimbia, wakati muda hana mashetani anakuwa hana nguvu hizo. Pia mtu mwenye mashetani hujigonga huko na kule Kwa nguvu kubwa na sometimes hata kujidhuru wenyewe lakini baada ya maombi flani watu hawa hutulia.
Swali langu ni kuwa watu hawa hupata wapi nguvu za kuweza kufanya yote haya? Je wanaigiza tu? Kama wanaigiza mbona hujidhuru sana? Kama ni matatizo ya kisaikilojia tu mbona hutibiwa kwa maombi na baada ya maombi hayo hali hukaa sawa?
Kwa lugha ya staha naomba tueleweshane🤝