Kwa upole sikupingi wewe ni mpole hapa JF. Ila ban tunapata watu hasa tukisahau sheria au kutosoma sheria. Watu wasiochangia si rahisi kupata ban.
Ila ban nyingine hutolewa ukimkosoa mtu mayai anayelelewa humu JF. Mfano ukikataa ujinga wa mtu mmoja humu mwenye ID mbili, anayejifanya mtu wa kitengo, ana matusi mengi na anapenda kutumia fungua na funga semi kwenye title za threads zake. Huyu ukimbishia kidogo anajifanya ana akili sana na wewe unaonekana POPOMA kisha mods wanaweza kukupa ban. Sio huyu tu, kuna jamaa alishawahi bishana na mtu wa kilingeni humu kuhusu ile app gani ilikuwa inatoa vocha, huyo jamaa alipewa ban.
Pia kuna watu wanakoseshwa ban mpaka nidhamu inakosa. Wanatukana matusi mazito na kudharirisha watu na kuachwa watambe.
Ukitaka kuepuka ban piga block kila unayehisi atakusababishia. Kuna watu unajua huyu kwa lugha hii, kauli hizi au mada hizi zinazonikera hata aandike nini hakiwezi nisaidia unapiga ban unabaki na mambo machache. Nawe utapigwa ban na asiyekuelewa.