Ambao hatuna Magari tukutane hapa!

Ambao hatuna Magari tukutane hapa!

Binafsi gari yangu ya kwanza ilikuwa kama bahati tu, wakati natafuta gari kuna msela alikuwa anafanya kazi NBC ameingiza X-TRIAL na bahati mbaya hana hela ya kutolea, ikabidi aniuzie Hari yake nkamwambia sina hela ya kutosha akaniambia nimpe 2M and the remaining ntampa 500k per month mpaka tutakapomaliza.
 
Mkuu, hiyo ndinga bado unayo? Nipe na mimi kwa mkataba aisee[emoji34][emoji34][emoji34]
Binafsi gari yangu ya kwanza ilikuwa kama bahati tu, wakati natafuta gari kuna msela alikuwa anafanya kazi NBC ameingiza X-TRIAL na bahati mbaya hana hela ya kutolea, ikabidi aniuzie Hari yake nkamwambia sina hela ya kutosha akaniambia nimpe 2M and the remaining ntampa 500k per month mpaka tutakapomaliza.
 
Vipi wakuu mko poa? [emoji23][emoji23]
Makonda wa daladala wanasemaje.....Mnadai mia au mnapotezea?[emoji41][emoji41]

Haya turudi hapa[emoji855][emoji855]

Leo asubuhi nilienda dukani, mara baada ya kuhudumiwa nikawa nasubiri mkate wangu wa chai anikabidhi....Akaja mama mmoja hivi anagari moja hivi nyeusi kali imepanda hewani, Tairi zake zote nne zipo juu juu yaani inanesa nesa tu[emoji856][emoji856]

Mama akashuka na kuja dukani huku gari inakimuungurumo fulani hivi cha chini chini wamiliki wanasema "sailensa"

Mama kajifunga kitenge na kisuruali mbano kipo ndani cheupe[emoji19][emoji19][emoji19] daah [emoji6][emoji6] lahaula.....[emoji1316]

Moyo umeniuma sana kwanini watu wanamagari mimi sina[emoji19][emoji19][emoji19] ...Nitawaeleza nini watoto[emoji34][emoji34]

Je waliyonayo wamefanya vipi ili kuyapata!? Je wote wamekopa? Je kwa biashara zao wafanyazo? Ni zipi hizo!? Je mitaji ya biashara hizo walitoa wapi? Urithi au waliuza mali za familia?[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Na sisi ambao hatuna magari tufanyaje ili tumiliki ndinga kali? Huwa unajisikiaje unakula lifti kwa mshkaji aliyekuzidi umri na ana ndinga kali wakati ww pia unanguvu zako?

Embu tujadiliane hapa, mbinu njia au ubunifu wowote utakao tusaidia kumiliki ndinga bhana[emoji34][emoji34][emoji34]

Nawasilisha mheshimiwa spika!!
Zamani nilikuwa nasemaga hivyo, ndugu zangu wakija na magar kunisalimia wakiondoka nachungulia dirishani, Leo hii siamini ni Mimi au, gari mbili zimepaki nje, na nyumba juu tena mtaa wa maboss, Mungu kasikia kilio,. Na wewe hipo siku yako.
 
Mkuu nipe madili na mm nipate gari[emoji34][emoji34][emoji34]
Zamani nilikuwa nasemaga hivyo, ndugu zangu wakija na magar kunisalimia wakiondoka nachungulia dirishani, Leo hii siamini ni Mimi au, gari mbili zimepaki nje, na nyumba juu tena mtaa wa maboss, Mungu kasikia kilio,. Na wewe hipo siku yako.
 
Ndugu, mishahara ya watu unaijua au unaiskia?? Afanye saving ya laki 5 per month???

Kama mshahara wako haukupi uwezo wa ku save laki tano basi jua wewe utakuwa masikinni milele unless u do something. Huwezi ku save laki tano alafu unafikiria kununua gari [emoji23].
Panda daladala mpaka ufikie uwezo wa kununua gari.
Unajua roughly mafuta kwa mwezi ni shilling ngapi?
 
Back
Top Bottom