Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Good morning jf....
Tusio na marafiki tukutane hapa😔
Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.
Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.
Wenye marafiki mnawapataje???