Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

jiunge na vyama
Mi mwenyewe sina chama hata kimoja ila rafiki nnao kama wawili huwa tunsaidiana na hata nikiwa nna shida kubwa nikiwacheki muamala unasoma haraka hawafikirii mara mbili
Wengine ninao ni wa stori na kumwagilia moyo tu 😂😂😂
 
Natafuta social capital kwanza
Kuna mengi,unaweza kuwa social lakini sio social eneough au labda ukawa too serious na maisha yako. Kwanza kabisa jifunze kuwa "mtu mwema" kuwa mtu wa kujitoa kwa watu. Wasaidie wenye uhitaji hata kama huna,watie moyo,wafariji na tenga muda wako kwa ajili ya watu. Jichanganye kwenye kwenye matukio kama misiba,harusi na sherehe mbalimbali,jifunze kujitoa huko.Tumia vipaji vyako kwa manufaa ya wote.Jiulize lengo lako la maisha hapa duniani ni nini? Kwanini unaishi? unataka watu wakukumbuke vipi? Jiulize siku ukifa nani na nani watakulilia?
 
Kuna mdada huwa napenda ile life style, weekends hupost status wapo kwenye coaster wanaenda kutembelea yatima yani wanavibe hao, usiku wapo pengine wanamwagilia moyo....napenda kwakweli ila mi sina
Kama mazingira unayoishi hamna watu sahihi,sio lazima uwe na marafiki wengi...Ni bora kutokuwa na marafiki kuliko kuwa na marafiki ambao sio sahihi,muhimu jifunze kuwa mtu mwema.Inatosha.
 
Me na wewe same same,naeza kuingia huko kwa group nikawa bubu. Hao wa zamani nao kila maisha yametutenganisha mnoo wengine sijui hata walipo. Yaani kupata rafiki mkashibana ni mtihani kweli kweli sijui hata nifanyeje [emoji26]
Kumbe yatatukuta wengi [emoji2][emoji18]. Nna marafiki lkn sio wa kindaki ndaki.
 
Ninajichanganya nao wapi yani nadhani pa kuanzia ndio sina
Kwa jinsia ya ke ni ngumu kiaina since bcoz mara nyingi mnakuwa mnahitaji rafiki mmoja tu maishani, tofauti na jinsia ya me unakuta kila category una mshikaji, mshikaji wa kunywa nae, mshikaji wa stori tu, mshikaji wa church or msikitini...na nk.....kwa ushauri kama unataka rafiki wa faida anza kujibrand kwa ukubwa utapata marafiki wa level kubwa mfano anzisha group la whatsap lipe title kubwa kama vile boss ladies utapata wa kufaana nae humo contents mtaanza kujadili jinsi gani mbadilishe laki kuwa billions n.k, Nb usifake. I hope umepata kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta vikundi vya kusaidiana ili endapo unasherehe au msiba wajumuike maana naona wasiwasi wako Ni kukosa company wakati wa shida au raha.Lakini huo urafiki unaosema wewe unaweza usiwe Kama unavyofikiria maana unawezakumpata rafiki ambaye atakua na wewe kwasababu anategemea kupata kitu fulani kutoka kwako hivyo akakusumbua hadi ukaona kero.
 
Marafiki mara nyingi ni watu tunaokutana nao sehemu ambazo tunafanya kazi au sehemu yoyote ambayo watu tunakutana kwa pamoja, lakini tukiwa tumekutanishwa na jambo fulani. Kupata marafiki ni rahisi sana. Kua mtu wa kwenda sehemu mbalimbali zinazokutanisha watu, penda kuongea na watu, lakini pia kua mtu safi usie na makuu. Taratibu utaona unapata watu ambao mtakua karibu zaidi
 
Nipo na notebook hapa hadi sasa nshaona wewe na naa mpo kama mimi, next week twende tu royo tua sasa make tunafanana
Ndo kilichobaki hicho. Mimi Nashukuru ni mtu ambaye najitoa sana, Yani dizaini shosti akiumwa nitaenda nimpikie uji mwenyewe sio kumuagiza mdada wake wa Kazi, nimfulie...najitoa sana, Nashukuru pia watu wa karibu wananipenda....shida ni Mimi, I can't keep them....Yani naona mapungufu Yao sana, nikijua umenisema nalegeza urafiki, afu hairudi hiyo....siwezi unafki kabisaaa.
Ndo naishia kuwa nipo nipo tu!
 
Good morning jf....
Tusio na marafiki tukutane hapa[emoji17]

Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.

Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.

Wenye marafiki mnawapataje???
Njoo hapa nipo
Ila kumbuka urafiki ni gharama
Are you ready to pay?
 
Back
Top Bottom