Ambiguity: nimekuta "MISSED CALL" yako!

kimanu

Senior Member
Joined
May 31, 2013
Posts
196
Reaction score
64
Wanajamii wanaojua kimombo, nina wasiwasi na hii kauli, pale mtu uliyempigia na "kumkosa" anapokupigia na kusema;
"....nimekuta MISSED CALL yako!"
Nijuavyo mimi, inapaswa kubadilika na kuwa MISSING CALL yako, kwani The "Missed Call" ilinayoonekana kwenye display ya simu yako ni past( wakati ule ambapo ulipaswa kuipokea)
NOW here it IS....
Help anyone?
 

Huo ujumbe nilioutilia rangi ya bluu ni sahihi kwa sababu, ukiangalia simu yako, kuna makundi (category) haya ya simu zilizopitia kwenye simu yako:

"Incoming calls" simu zote zilizoingia kwenye simu yako (zilizopokelewa na zisizopokelewa)
"Outgoing calls" simu zote zilizotoka kwenye simu yako
"Missed calls" simu zilizoingia kwenye simu yako lakini hazikupokelewa.
"All calls" simu zote (in and out)

Sasa kama mimi nikiangalia simu yangu kwenye kundi la missed-calls na nikaona moja ya zile missed-calls ni ya kwako, ni sahihi kukueleza kuwa "nimekuta missed-call yako."

Haya, nimesaidia au ndio nimekoroga zaidi?
 
nimekupata BUT kauli yako kwa aliyekupigia kwa wakati huu inapaswa kuonesha wakati uliopo
 
nimekupata BUT kauli yako kwa aliyekupigia kwa wakati huu inapaswa kuonesha wakati uliopo

Kinamu kauli hiyo haiwezi kuwa ya wakati uliopo kwa sababu unapokuwa unaongea na mtu huyo, unamjulisha habari ya wakati ule uliompigia na ukamkosa. Kwa hiyo njeo hiyo lazima isawiri wakati uliopita, missED call!
 
Njeo itazingatiwa zaidi kwa kuzingatia mda ambapo tukio lilitendeka kwahiyo hapo itakuwa sahihi ukisema"Missed call"kwa kuwa tukio limekwisha tendeka
 
hapa nasisitiza matumizi ya Quotation Marks na masuala ya Passive na active cases . let's go!
 
Yeye(mtoa maada)alikuwa anataka iwe MissING call kitu ambacho si sahihi! Hivi umwambie mtu nimekuta "Missing call" yako wakati tayari umeikuta hata kama ni sekunde tano zimepita bado itakuwa kwenye wakati uliopita! Haijakaa vizuri hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…