Amchoma Kisu Mpenzi wake shingoni baada ya kutishia kumuacha

Amchoma Kisu Mpenzi wake shingoni baada ya kutishia kumuacha

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
David Njuguna (32) mkazi wa Githurai nchini Kenya ametiwa mbaroni kwa kudaiwa kutaka kumuua mpenzi wake Mary Wangechi ambaye inadaiwa alimtishia kumuacha baada ya kugombana.

Njuguna ambaye kwa sasa kesi yake inarindima katika Mahakama ya Makadara iliyoko jijini Nairobi anadaiwa kumchoma kisu cha shingo Mary ambaye amesema amemuacha baada ya Njuguna kutoweka nyumbani kwa wiki nzima bila kutoa taarifa.

Hakimu Mwandamizi, Gerald Mutiso ameambiwa kuwa Njuguna alikuwa anaishi nyumbani kwa Mary katika mtaa wa Githurai, lakini baadaye alitoweka nyumbani kwa wiki nzima bila kutoa taarifa yeyote, aliporejea Juni 11, 2023 akaulizwa aseme alipokuwa jambo ambalo lilizua ugomvi.

Ugomvi ulipopamba moto Njuguna alimchoma kisu cha shingo Mary na kutokomea kusikojulikana. Wangechi alijiburuza hadi nje ya nyumba akaomba msaada kwa majirani ambao walimkimbiza katika kituo cha afya kilichopo karibu.

Njuguna alikamatwa na kufikishwa mahakamani lakini amekanusha mashtaka dhidi yake na alipewa dhamana. Kesi hiyo imepangwa kuendelea Jumatatu ya Julai 10, 2023

MWANANCHI
 
Ingekua huku kwetu, hiyo dhamana angeiskia kwenye bomba.
Angesota mahabusu mpka apauke
 
Njuguna apewe kisheri chake
20230513_224328.jpg
 
Back
Top Bottom