PROCESSOR
Inategemea na kazi unayofanya hata na software unayotumia. Kwa jumla kwa kazi ambazo ni graphic oriented AMD inatajwa kuwa imejielekeza zaidi huko. Mfano AMD na HP huwa wana projects wanazoshirikiana kuandaa workstation. Sinema ya Shrek imetengenezwa kwa software ya Autodesk Maya katika workstation (powerful computers) za HP zenye processor za AMD. Inategemea pia na uwezo wa processor husika. Mfano hapa ninapoandika post hii natumia laptop yenye AMD Turion X2 ni duo core nzuri lakini huwezi kuilinganisha na Intel Core 2 duo au Intel Core i3 au i5 au i7 ambazo ni more powerful. Intel pia wamekuwa na rekodi ya kufanya mapinduzi ya haraka kiteknolojia kuliko AMD. AMD wamekuwa na sifa ya kufanya reverse-engineering ya processor za Intel. Developers wengi wa software huwa wanaandaa programs zao vichwani wakiwazia processor za Intel. Mfano kuanzia Adobe Creative Suite 4 (CS4) ilitajwa kama "It will be Intel only." Hii ilikuwa ni ujumbe maalum kwa watu wa Macintosh wenye processor za Motorola (PowerPC G1-G5) kuwa "wanapigwa chini." Hii haimaanishi kuwa AMD haiwi supported, yangu ni AMD kama nillivyosema na natumia Adobe CS4.
Macintosh kuanzia OS yao ya Leopard wameanza kutumia processors za Intel (siyo AMD)!! Sasa wako na Snow Leopard na ni Intel only si AMD wala PowerPC. AMD wanatarajia baada ya michache watoe CPUs ambazo ziko merged na GPUs (Graphic Cards), zitakuwa bomba sana. Software kama Adobe Premiere CS5 wanatumia teknolojia wanayoita Mercury Engine ambayo inafanya kazi kwa nguvu kweli kwa msaada wa multicore-CPUs na GPU kwa pamoja, ni very poweful combination. Hata hivyo ili kufanikisha hili Adobe Premiere CS5, After Effects CS5, Encore CS5 na Adobe Media Encoder CS5 ni 64 bit only. Hivyo watu kama mimi wenye 32 bit OS tumeshaachwa!!! Kumbuka 32 bit OS huishia RAM 4 GB lakini 64 bit inakwenda mbali zaidi, najua kuna kompyuta zenye RAM zaidi ya 12 GB!! Actually ni zaidi ya hapo. Google HP Z800.
GRAPHIC CARD
Nvidia wamekuwa mstari wa mbele kuliko ATI katika mapinduzi. Najua pia ATI Graphic Cards ni nzuri kwa Gaming kuliko Nvidia (lakini game gani unacheza bwana hadi uone Nvidia iko chini?). Pia inategemea na version ya Graphic card na drivers. Nvidia CUDA na Nvidia Quadro ni very powerful graphic cards. Watengeneza software pia huweka vichwani mwao Nvidia japo haimaanishi ATI haiwi supported. Kuna maneno mengi sana ya kuchanganya wanunuzi.
USHAURI WANGU,
- Fahamu kwanza utataka kuitumia kompyuta kwa kufanya nini na software zipi utafanyia kazi
- Hakikisha kompyuta yako ina RAM ya kutosha zaidi ya 3 GB na Hard Disk ambayo ni fast ili usije kuwalaumu Adobe au Nvidia au AMD
- Kama utalazimika kuchagua basi Chagua Intel na Nvidia, motherboards sina detail nyingi, nahitaji kufanya research
- Fahamu namna ya kufanya configuration (kama ni lazima) ya kompyuta ili iendane na software zako
- Usitishwe sana na mabishano ya Intel na AMD, ni sawa na watu kubishania scientific calculator wakati wengi wao wanaishia kwenye hesabu za quadratic equations
Ni hayo tu.