Dejane
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 50,587
- 71,492
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
keshanunua Ventilator kumi lakini hapendi show off. yooooooooooooooooooooooooooooooohmwambie na Alli kiba mfalme wa bongo fleva
Kwenye uhasibu kuna principle moja muhimu tunaiita prudence....yani kadiria mapato kwa kiwango kidogo ambacho kinaweza kufikika pasipo na shaka ila unapokadiria hasara au matumizi basi kadiria kwa kiwango kikubwa sana.
Haya mambo ya kutegemea kipato kutoka kwa followers kibongobongo ni ngumu mno, sema sepetu alizindua sendo zake zile akidhani followers watakua mtaji ila alitoka kapa wakaanza kuziuza mpaka stejini na bado hazikuuzika hadi akaacha. Pia kwa idris ulikuwa hivi hivi.
Katika hao followers laki 6 wa Roma na laki 7 wa stamina kuna followers milioni tu maana wengi waliomfollow moja wao basi wamemfollow Mwenzake.
Katika followers hao milioni ni vema wangeanza na lengo dogo hata wapate mchango wa buku kutoka kwa followers elf 10,
Wasije kufanya kosa la kuwaona followers ni mgodi utaotema fedha, hapa watakua wamekosea sana maana followers wengi ni vijana tu wadogo wa sekondari na vyuoni ambao kwasasa wapo majumbani hata hela za poket money hawana, ila pia kuna kundi kubwa la followers ambao nivijana waliomaliza vyuo wasio na ajira, na hata kundi la vijana wenye ajira basi wana minyororo kwenye mishahara yao kusaidia ndugu zao, ni followers wachache ambao wapo vizuri kiuchumi maana wengi wao hawanaga muda na Instagram wanakuaga bize na kazi au biashara.
Kwa mtazamo tu naona wawe na lengo jipya la kukusanya milioni 10 kwanza kutoka followers elf 10 wataochangia buku buku, najua hata hicho kiasi kikitumika kununulia barakoa kitasaidia Jamii kuliko huko kwenye milioni 300 ambako ni ngumu sana kufikia
Kichwa chako kimebeba sisimizi badala ya ubongoHii ndo Michango ya kuisaidia jamii bila janjajanja ya kutafuta misifa.. Diamond si mbaya Kuiga mawazo ya kibunifu kama haya
Si kukusanya watu 20 Unapawa bahasha umeweka 20k unasema umewasaidia watu 500 kuwalipia kodi, Hakuna atakae kuamini kila mtu atakuona mjanja mjanja,na kutafuta kik na misifa
huu ndo maana ya ukioo wa jamiiKwa Jinsi Ambavyo Nimeona Watu Wengi Mmeupokea Wimbo Wetu Wa KAKA_TUCHATI Na Kuvutiwa Nao,
Nimewaza Jambo Fulani, Mimi Nina Followers Hapa Instagram Laki Sita 600K, Na Staminashorwebwenzi Ana Followers Laki Saba 700K
Sisi Ni Wasanii Masikini (Tusio Na Kipato Kikubwa) Lakini Tumejaliwa Vipaji Na Utajiri Wa Watu (Mashabiki)
Tukisema Kati Ya Hao Tuchukue Followers 600K tu, Kama Kila Mmoja Kutokana Na Kuguswa Kwake Na Kuupenda Na Kuufurahia Wimbo Huu KAKA_TUCHATI Nikiomba Achangie Tsh. 500 tu!! (Mia Tano Tu) Kwa Ajili Ya Project Hii, Na Kama Wote Watu Laki Sita Watachangia Basi Itapatikana Tsh 300M (Milioni Mia Tatu).
Mashine Moja Ya Ventilator Gharama Yake Ni Tsh. 100M
Hivyo Basi Tukifanikiwa Kupata Hizo Milioni 300, Tuna Uwezo Wa Kununua Ventilator 3 Na Zitasaidia Kuokoa Maisha Ya Ndugu,Jamaa Na Marafiki Zetu Wengi Kwenye Janga Hili La Corona Covid_19 Hasa Mikoani Ambako Ndio Kuna Uhitaji Zaidi!! .
Lengo Letu Kama #Rostam (Roma Na Stamina) Ni Kusaidia Jamii Yetu Kama Yalivyo Maudhui Ya Nyimbo Zetu Nyingi Na Kuacha Alama Chanya Kupitia Sanaa Tunayoifanya Hasa Kwenye Huu Wimbo Wetu Mpya Wa KaKa_Tuchati Ambao Umetokea Kupokelewa Vizuri Sana!! Tunaamini Mashabiki Zetu Na Hata Wale Wasio Mashabiki Zetu ila Wamependa Tulichokifanya Katika Hili Mna Uwezo Wa KutuSupport Kulifanikisha Hili Zoezi.
Rostam Tunataka Kununua Mashine Ya Ventilator Angalau Hata Moja Na Hii Ndiyo Itakuwa Challenge Ya Wimbo Wetu KaKa_Tuchati
Mashabiki Wa Muziki Na Sanaa Yetu/Viongozi Wa Serikali/Viongozi Wa Dini/Wanasiasa/Wafanyabiashara Na Wajasiriamali/Wanafunzi/WasaniiWenzetu na Wadau/Wanaharakati/MashirikaBinafsi/TaasisiMbaliMbali/KampuniMbaliMbali/ Na Hasa Vyombo Vya Habari Na Yoyote Aliyeguswa Na Hili Ningeomba Tuungane Kwa Pamoja Kulifanikisha Hili Zoezi Na Kuusambaza Ujumbe Huu Wa Hii Challenge Ya Rostam
KaKa_Tuchati Ventilator_Challenge .
Na Tuisaidie Jamii Yetu Katika Hili La Kuokoa Roho Za Ndugu Zetu Kwenye Janga Hili La Corona!! .
NB - Hata Ukiwa Na Kiasi Pungufu Na Tsh 500 Utakuwa Umechangia Pia Na Tutapokea Na Kukushukuru, Na Hata Ukiwa Una Kiasi Cha Zaidi Ya Tsh 500 Tutashukuru Na Utakuwa Umechangia Pakubwa Zaidi.