Salaam kwenu nyote.
Ninaomba ushauri wenu kwenu Kaka zangu na Dada zangu. Mimi ni binti.
Nimekutana na changamoto katika mahusiano yangu. Kisa ni hiki.
Nilikuwa katika mahusiano na kijana mmoja kwa takriban miaka 4. Baadae ikaonekana ni vema tufahamishe mahusiano haya ngazi ya wazazi. Kijana alikuja nyumbani kwa tararibu zote na kupangiwa mahari. Wakati wote huo mimi na kijana tuko vizuri na mawasiliano kwa hakika yalikuwa mazuri mno. Naweza kusema hakukuwa na jambo au tatizo baina yetu na mwenzangu ambalo labda lingekuwa kikwazo.
Hata hivyo, week moja kabla kuelekea siku ya mahari mwenzangu alinifahamisha kwamba wamehairisha kuja nyumbani kwetu sababu familia yake imeona gharama walizopangiwa ni kubwa. Naye alishikilia msimamo kwamba anaungana na familia yake.. Nilijitahidi sana kumweleza kwamba waje na gharama walizojiandaa nazo lakini haikuwezekana tena kwa mwenzangu. Ni kama alishaamua kusitisha jambo hili na mahusiano yote kwa ujumla na kwa hivyo sikuweza kubadili chochote kutokea hapo.
Nimejitahidi mara kadhaa kutaka kujua iwapo kuna sababu nyingine ya sababu hiyo lakin mara zote mwenzangu amekuwa akijikita katika sababu tajwa hapo juu. Hata ninapomuuliza mwenzangu juu ya nini kinachoendelea mpka wakati huu bado hanipi majibu. Kimsingi, inaonekana hakuna mahusiano tena kwa sasa.
Ninaumia kwa namna mambo yalivyoenda na yalivyohitimishwa kwa namna isiyotarajika. ona ni kama ndoto, labda nipo ndotoni lakini ni ukweli ambao watu wanapitia. Nipo katika wakati mgumu mno, ukizingatia kwamba taarifa za jambo hili ziliwaslishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Nimekuja kwenu naomba ushauri, nahitajika kufanya nini ili niweze kuchukuliana na changamoto hii? Kuna wakati nashindwa kama binadamu naogopa kumfuru Mungu wangu. Nashindwa kusahau na namkumbuka sana kila wakati.
nafdat dada yangu mpendwa;
Pole kwa changamoto hii.
Najua unapitia kipindi kigumu sana.
Huenda mwenzio aliiuwa hajamaanisha zaidi aliona amepata mteremko wa kupata free p.
Wanawake mnapitia magumu sana.
Nikushauri kuwa uwe jasiri, idharau aibu.
Mimi ni Mkristo kuna mstari huwa unanitia nguvu naomba kushea;
(5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
Wafilipi 2:5
6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
Wafilipi 2:6
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
Wafilipi 2:7
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Wafilipi 2:8
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
Wafilipi 2:9
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
Wafilipi 2:10
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Wafilipi 2:11)
Maneno hayo maana yake ni kuwa Yesu ambaye alikuwa na utukufu, kuna wakati alikubali kuaibika na hakuona kuwa ni tatizo bali aliutazama utukufu mpya ujao.
Hakukwepa aibu bali aliikabili ndipo alipoishinda aibu Mungu alimuadhimisha mno au alimpa utukufu mpya.
Dada iiabili aibu huku ukimsubiri mume wako bora kabisa.
Mungu atakupa kitu bora kabisa..tulia.
Yatunze haya maneno.