Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini Taifa, Ameir Hassan Ameir, amesema kuwa endapo wananchi wa Zanzibar watampa ridhaa ya kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika uchaguzi ujao, atahakikisha kila mwananchi wa Zanzibar anapokea mshahara wa shilingi 500,000 za Kitanzania kila mwezi.
Ameir ametoa kauli hiyo leo katika kikao kazi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa ldara ya Habari (Maelezo) Zanzibar, kilicholenga kujadili utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 pamoja na matarajio ya ilani ijayo ya mwaka 2025-2030.
Akizungumzia mpango huo, Ameir amesema lengo ni kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto za umasikini, ukosefu wa ajira na utegemezi miongoni mwa wananchi wa Zanzibar, hasa vijana na wanawake.
"Ni wakati sasa wa kujenga Zanzibar yenye heshima, usawa wa kiuchumi na mustakabali bora kwa kila raia, bila kujali hali yao ya sasa," alisema Ameir.