Amekimbia mkorofi amepata mkorofi!

Amekimbia mkorofi amepata mkorofi!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu tuchukulie kwamba umeachana na mpenzi wako. Pamoja na kwamba huyu mpenzi ana ukorofi wake, lakini kilichoharakisha hadi ukaamua kuachana naye ni mpenzi mwingine mpya ambaye unaamini kwamba ni bora zaidi.

Unaachana naye na kuanzisha uhusiano na huyu ambaye unaamini kwamba, ndiye hasa anayekufaa. Lakini kwa muda mfupi tu, huyu mpenzi mpya anaanza ukorofi. Unagundua kwamba, ana matatizo na ni mkorofi mara mia zaidi ya yule mliyeachana.

Hebu fikiria, ulishatamba kila mahali kwamba, sasa umepata mpenzi wa maana. Hebu sema, utafanya nini katika mazingira kama hayo?

 
Hapo chakufanya huna unajipanga upya sio lazima mpaka akutoe roho,na ndio mana watu wanasema usinyie kambi kabla hujaiama,sio vizuri kuongea sababu binadamu yoyote sio wakumchukulia dhamani 100% muhimu ukimpata mwanamme muhimu nikuomba mungu muwena maelewano na muheshimiane.....
 
Back
Top Bottom