Amekuibia mume

Amekuibia mume

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775

MUME AMEKUIBIA
Mama Joti! Mama Joti!, hebu njoo mara moja
Wala usije na kiti, naharaka sitangoja
Tena uvae thabiti, ukatazame vihoja
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Niliyoyaona huko, kuyasema ni aibu
Kaibiwa mume wako, na rafiki yako Tabu
Ajifanya dada yako, huku anakuadhibu
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Katika mihangaiko, ndipo nikapita Baa
Nikawakuta mwenzako,pembezoni wamekaa
Walishana kwa vijiko, supu ya pweza na taa
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Nikajibanza pembeni, ili kuwahakikisha
Nikawaona machoni, hapo nikathibitisha
Tabu na wako mwandani, penzi wameliotesha
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Sikuacha kuwawinda, kwa mwendo wa nyatu nyatu
Mpaka gesti wakenda, kule ghorofa ya tatu
Kulisakata kandanda, kwa kujifutua futu
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Kweli kinguoni mwako, kikulacho ndani ndani
Wakati wala ukoko, wao wapo zao pwani
Wanavifanya vituko, wewe uko taabani,
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Kisha nikapata wazo, ujumbe kukuletea
Habari yenye mjazo, ya yote yaliyotokea
Nawe ujue tatizo, vipi utalitatua?,
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Unakumbuka lakini, ulichomfanya jeni
Aliposema jamani, bwana wake hamuoni,
Ukambeza moyoni, kumbe unae chumbani
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Basi mimi naondoka, bali nyamaza kulia
Wawahi wasije toka, ukweli ukapotea
Tena ufanye haraka, hata mbio kukimbia
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Malipo ni Duniani, akhera kuesabia
Jambo hili aminini, ndugu zangu nawambia
Kumuogopa MANANI, ndio mpango sawia
Mwivi uliyemfuga, mume amekuibia.

Mshairi Machinga,
mfaumehamisi@gmail.com,
0716541703/0677620312,
Dar es salaam,Kariakoo.
 
Idd Ninga,

Punguza kiherehere,ninga wauwa ndoa
Usiigonge kengere,wengine watasikia
Kula wali njegere,NATO maji gugumia
Raha ya mume wanne,tabu ni namba tatu

Ya matumizi naacha,kwa Jane hadi kwa tabu
Siwavalishi chachacha,ndo uone maajabu
Na sivujishi pakacha,mchukuzi sina tabu
Raha ya mume wanne,tabu ndio tatu namba
 
Idd Ninga, Umekuwa ukiandika mashairi bila kuchoka je,yanakulipa au unaandika kwa kujifurahisha tu....???
 
Back
Top Bottom