Ameniomba turudiane nimemkatalia!

Jakubumba

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2011
Posts
1,624
Reaction score
501
Nilikuwa na girl friend tangu 2002 hadi 2006. Tulipendana sana ingawa hatukuwa na kipato chochote maana tulikuwa wanafunzi, tulipohitimu form six mwenzangu alianza kubadilika kitabia na nilipomuuliza akawa anakana kabisa,ila mwisho wa siku mambo yakawa hadhalani ana uhusiano na mwanajeshi na ana mpango wa kumuoa! Nilimsihi nampenda tuvumilie tutakuwa na maisha yetu ila akakataa na akaniambia amisha mpenda mtu mwingine. Kwa kuwa huwa naamini mapenzi hayalazimishwi nikajipa moyo na kusonga mbele! Mungu si athumani akanijalia nikapata chuo USA nikawa nimeondoka tz hivo machungu sikuyapata sana maana nikawa niko mbali hata simuoni anavyofurahia penzi lake jipya! Ni miaka minne sasa imepita, nilishtuka sana juzi baada ya kuona sms yake kwenye simu yangu ikinisihi kumpigia! Sikusita nikampigia: kikubwa zaidi akawa ananiomba msamaha turudiane aliko hafurahii maisha! Wanajf! Mie huwa nina msimamo sana ktk maisha yangu, jibu nililompa ni kuwa asijisumbue kuomba msamaha maana sitamkubalia kabisa! Je nina kosa? Ukweli ni kuwa ninatafuta mchumba ila siko tayari kurudi nyuma kwa mtu alienitenda nataka kusonga mbele!!!
 
songa mbele na usirudi
tafuta atakaye kupenda na unayempenda.
 
Kumwambia mtu ukweli sio kosa labda kama unamfeel hapo ndo utakuwa unajikosea mwenyewe!
 
Kumwambia mtu ukweli sio kosa labda kama unamfeel hapo ndo utakuwa unajikosea mwenyewe!

ukweli nilikuwa nampenda ila yeye kunitamkia wazi kuwa ampenda mtu mwingine iliniumiza sana! Mawaidha ya wazazi wangu yaliniponya na maumivu! Kiukweli sitokubali kurudiana nae maana atakuja anitende zaidi ya alivyotenda
 
Naanza na Dongo:
Jina lako haliko kwenye uke wala mme, avatar yako ya ke, maswali unayouliza ya me!
Mi nashangashangaa tu kwenye avatar yako, ujui watu wanaweza maliza matatizo yao kwenye avatar yako?

Ushauri:
Achana na hiyo mtu kabisa tena mwambie ushampata mbadala yake!
 
Shukrani kwa ushauri wako! Mimi ni me! Sio ke!
 
Pole dada/kaka yangu..ila umenikera sana na tabia ya kuweka picha ya ke wakati maelezo yako yanaonyesha ni me...plse, siyo vizuri na hii imekuwa tabia siku hizi hapa JF kwa baadhi ya member kujipachika jinsi/sex ambazo siyo zao. Sijui mnafaidika nini na ku-hide jinsi zenu.
Kwa kweli nilitamani kukupa ushauiri ila kwa picha uliyoweka unaonyesha hauko serious....
 
huo ndo msimamo wa kiume hamna kugeuka nyuma,tena mwambie asahau.
 
endelea na maisha yako, acha kigugumizi na misimamo ya sitaki-nataka
 

samahani sana nitabadilisha avator yangu mkuu!
 
pole badili avatar yako kumbe we dume afu unajiweka picha ya kike ili iweje
 

Yap! Huo ndiyo msimamo. Hakuna kula matapishi!
 
Kwani kumsamehe mtu kama huyo lazima mrudiane? Mi nakushauri umsamehe, lakini msirudiane kamwe....!
 
ukweli nilikuwa nampenda ila yeye kunitamkia wazi kuwa ampenda mtu mwingine iliniumiza sana! Mawaidha ya wazazi wangu yaliniponya na maumivu! Kiukweli sitokubali kurudiana nae maana atakuja anitende zaidi ya alivyotenda

Sasa Jakubumba ndugu yangu, kumbe hutaki kurudiana nae kwa hofu kuwa anaweza kukutenda tena? Kwani huyo utakaempata una uhakika gani kwamba hatokutenda? Mi nakushauri usirudiane nae endapo humpendi na mapenzi yako kwake yashaisha.....!
 


10,000% right Mzee! Katoka maisha ya ujanafunzi akaingia jeshini sasa anataka ya ughaibuni. Pengine kwake wanaume ni chombo tu cha kupata maisha mazuri sio maagano ya kuishi kwa hali zote,raha na shida!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…