Yaani we unanitia hasira mbayaaa..ingekuwa ni mimi hata hapa jf nisingetia maguu kuja kuomba ushauri. Tena kwa jinsi alivyokuacha kwa nyodo mshenzi huyo wallah mi hata hiyo simu nisingempigia.
Huyo hana mapenzi ya kweli bali yuko kimaslahi zaidi. Alikuona huna kitu akakuacha kwa nyodo na dharau, kaenda huko ashatumika sana then mambo yamekuwa magumu ndio anakuja kwako akuletee wewe makombo nyambafuuu tena we ingekuwa mdogo wangu ningekukata mambataaa...
Ukirudiana na huyo demu utakuja juta maisha yako yote, we mshukuru Mungu amekuepusha na huyo nyang'au mwenye tamaa ya kufa mtu. Mungu akaamua kukurudishia heshima yako mtoto wa kiume akakutoa machungu na kukupa katrip ka USA, sasa kama unataka kumfanya Mungu mjinga rudiana na hilo gubeli uone cha moto, atakutenda zaidi ya hapo mwanzo.
Tena we mi nahisi umezubaa sana, yaani tangu 2006 mpaka leo bado hujapata demu mwingine na watoto wote wazuri namna hiyo mdogo wangu? Wapo watoto wengi tu wazuri sana, wasomi, na wenye maadili safi kabisa wanatafuta watu makini wa kuwaoa, ni suala la kutulia tu na kuwa makini bila kusahau kumwomba Mungu.