Ameniomba turudiane nimemkatalia!

Sasa Jakubumba ndugu yangu, kumbe hutaki kurudiana nae kwa hofu kuwa anaweza kukutenda tena? Kwani huyo utakaempata una uhakika gani kwamba hatokutenda? Mi nakushauri usirudiane nae endapo humpendi na mapenzi yako kwake yashaisha.....!

Hata akitendwa na huyo mpya itakuwa ni mwanzo kwa huyo lakini kutendwa tena ni kujitakia.
 
10,000% right Mzee! Katoka maisha ya ujanafunzi akaingia jeshini sasa anataka ya ughaibuni. Pengine kwake wanaume ni chombo tu cha kupata maisha mazuri sio maagano ya kuishi kwa hali zote,raha na shida!

asante mkuu! Msimamo wangu ndo huo!
 
Hata akitendwa na huyo mpya itakuwa ni mwanzo kwa huyo lakini kutendwa tena ni kujitakia.

ur right mkuu! Hicho ndo nilifikilia nikawa naona ni bora anitende mwingine ila sio yeye tena! Dunia sasa hivi imeharibika sijui labda ana nia gani ya kunitaka tena, anyway yakimwagika hayazoleki! Thanks sana!
 

...songa mbele Mkuu usiangalie nyuma haikuwa bahati yako huyo...labda kasikia mahali kwamba mambo yako ni bomba sana ndio anaanza kujipitishapitisha. Mie sioni kosa lako katika hili.

 
Mkuu nowdays usimlazimishe mwanamke la sivyo atakutesa sana, achana nae kabisa mpotezee na songa mbele wanawake wapo wengi sana na wenye tabia nzuri,alafu anaona upo huko ndio anakutaka anajuwa lazima umpelekee mapene haha achana nae huyo hamna mpya kabisa..
 
Duh! nilikuwa wala sijaiangalia avatar mpaka ulipoandika Mkuu.


Hahaha mkuu ni dume huyo mimi mwenyewe nilijuwa mwanamke...Sasa nashangaa why ameweka avatar ya mwanamke
 
Mdau nasema huyo si demu. Yani HAFAI.
Hata kama dunia nzima kukawa hakuna tena mwanamke na amebaki peke yake, bado mfanye DADAKO kuliko kumwoa.hafai kuwa mpenzi huyo.
 
Yaani we unanitia hasira mbayaaa..ingekuwa ni mimi hata hapa jf nisingetia maguu kuja kuomba ushauri. Tena kwa jinsi alivyokuacha kwa nyodo mshenzi huyo wallah mi hata hiyo simu nisingempigia.

Huyo hana mapenzi ya kweli bali yuko kimaslahi zaidi. Alikuona huna kitu akakuacha kwa nyodo na dharau, kaenda huko ashatumika sana then mambo yamekuwa magumu ndio anakuja kwako akuletee wewe makombo nyambafuuu tena we ingekuwa mdogo wangu ningekukata mambataaa...

Ukirudiana na huyo demu utakuja juta maisha yako yote, we mshukuru Mungu amekuepusha na huyo nyang'au mwenye tamaa ya kufa mtu. Mungu akaamua kukurudishia heshima yako mtoto wa kiume akakutoa machungu na kukupa katrip ka USA, sasa kama unataka kumfanya Mungu mjinga rudiana na hilo gubeli uone cha moto, atakutenda zaidi ya hapo mwanzo.

Tena we mi nahisi umezubaa sana, yaani tangu 2006 mpaka leo bado hujapata demu mwingine na watoto wote wazuri namna hiyo mdogo wangu? Wapo watoto wengi tu wazuri sana, wasomi, na wenye maadili safi kabisa wanatafuta watu makini wa kuwaoa, ni suala la kutulia tu na kuwa makini bila kusahau kumwomba Mungu.
 

Mganga njaa huyo achana nae!!!
:lol::lol:Mkuu kama wewe ni wa kiume and then unatumia avata ya kike duuh napata shaka.:A S embarassed::A S embarassed:
 
Piga chini, wapo madrmy wengi wanao igiza maisha kama huyo, piga chiniiiii
 
Huu ni ushauri bomba sana, lkn kama tu yeye ni mwanaume rijali! Hivi mwanaume na akili timamu unaweka avatar ya kike! Japo ni uhuru wake hata akivaa sketi! Labda ana kasoro ambazo hata demu mwenyewe ameona ni wa kuchezea akili.
 
Umeshamaliza mchezo mzee safi sana.Ila watu wenye msimamo hawatakagi ushauri.All in all you made good decision
 
mimi naona umsamehe kwa aliyokutendea lakini msirudiane kwani hana mapenzi ya dhati, pili ninaona ww tayari unajibu coz umesema ww ni mtu wa msimamo, endelea kuwa na msimamo huo ila umwondoe rohoni coz ukimweka moyoni utaziba nafasi ya mchumba mpya mungu atakaye kupa!
 

"Maisha ni mbele kwa mbele usirudi nyuma - ukirudi nyuma utageuka jiwe" Dr. Remmi Ongala
 
hafai huyo-kama ameshakupotezea then kaona mambo yako yanaweza kunyoka ndo anajileta,
mpotezee,mwambie ulishamsahau
 
Msamehe bure, kuna siku utaikumbuka hiyo oppotunity na hutaipata. Msamehe bure and you will never regret
 
Jacubumba - Pole Sana! Mapenzi ya shule ni mara chache sana kufika mbali. Mambo yamebadilika siku hizi na ni rahisi sana watoto wa kike kupata vishawawishi toka kwa wanaume wenye vipato zaidi ya age/college mates. Uamuzi ni wako na umeshaufanya....Songa Mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…