Amenitelekeza hotelini, kisa sikwenda na salio la kumpatia

Amenitelekeza hotelini, kisa sikwenda na salio la kumpatia

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Hivi karibuni, nilipata mualiko kwa kamchepuko kangu, ambaye anadai ana ujauzito wangu.

Ikabidi niwe mzalendo na kuamua kufunga safari mpaka mkoa aliopo.

Baada ya kufika, nikatafuta eneo la malazi; nikapiga maji kidogo ili kuondoa uchovu, nikawa nimeagiza kinywani nakunywa taratibu hapo chumbani, huku nikimsubiri huyo mwali.

Baada ya muda nikapokea ujumbe wake mfupi, wa kutaka kujua sehemu niliyopo pamoja na chumba namba.

Baada ya kama nusu saa hivi, akawa amefika; nikiangalia tumbo lake naona limekuwa 'flat', nikajiuliza atakuwa amefyatua nini?

Basi tukawa tunazungumza; ila malalamiko yake mengi ni kutaka hela tu, mbaya zaidi alitaja mpaka kiasi; mi nikamwambia kwa sasa sina hicho kiasi, baadaa ya siku mbili nitakutumia.

Akawa mkorofi kweli, akawa hataki kunisikiliza; nikijaribu kumpatia 'romance' anapangua, baadaye ikabidi nitumie nguvu kidogo ingawa tulikuwa tunasukumana na hatukuweza kufanya lolote.

Ile naangalia tumbo vizuri, kumbe amelibana ili lisionekana; hapo hapo akili ikaniingia kichwani, huyu hayuko tayari kuwa na huu ujauzito.

Katika kuvutana vutana sana, nikaona isiwe shida, asije akapiga kelele nataka kumbaka; ile namuachia upenyo, akanyanyuka haraka nakufungua mlango na kutoka nje mpaka mapokezi, na kuanza kujisitiri vizuri ili aondoke.

Nampigia simu, anasema 'usinitafute tena na maamuzi ya huu ujauzito ninao mwenyewe'; mi nikamwambia sawa haina shida.

Baadaye ikabidi nitoke nje, ili nikabadilishe mazingira; napita pale mapokezi wakawa wananitazama kweli, nikasema kimoyo kimoyo sijui yule binti amewaambia kitu gani.

Niliporudi kulala nikawa sipati usingizi; ikabidi nitafute kampani huko 'online'; angalau aje anifariji kwa yaliyotokea.

Kusema kweli, si kila mwanamke ana sifa za kupewa ujauzito; najuta kupoteza mbegu zangu pale.​
 
Hivi karibuni, nilipata mualiko kwa kamchepuko kangu, ambaye anadai ana ujauzito wangu.
te kampani huko 'online'; angalau aje anifariji kwa yaliyotokea.

Kusema kweli, si kila mwanamke ana sifa za kupewa ujauzito; najuta kupoteza mbegu zangu pale.​
Unajuta kupoteza mbegu una uhakika gani kama anaujauzito wako? Au una fata kauli yale?
 
Back
Top Bottom