Amenitelekeza hotelini, kisa sikwenda na salio la kumpatia

Amenitelekeza hotelini, kisa sikwenda na salio la kumpatia

wanawake ni wauaji sa apo anataka aue kiumbe kina makosa gani? we kalia kuimba nani kama mama huenda nawe ulizaliwa kibahati mbaya,ile mimba kutaka kuchomolewa tu ikagoma ndo ukazaliwa
 
Mkuu kuwa makini yawezekana anatumia triki uyo kukupiga virungu ili ajipatie riziki kupitia wewe wadada wa siku hizi ni majinamizi kabsa kuwa makini
 
Fala mwingine huyu....
Swali; umeajiriwa na kampuni ya vinywaji vikali (pombe), wamekuja kwako kuomba ushauri kama mtu mbobezi wa masoko, wafanyeje fanyeje ili kwa siku mzigo wa kreti 10,000 uishe?

Toa jibu.​
 
wanawake ni wauaji sa apo anataka aue kiumbe kina makosa gani? we kalia kuimba nani kama mama huenda nawe ulizaliwa kibahati mbaya,ile mimba kutaka kuchomolewa tu ikagoma ndo ukazaliwa
Wapo wenye huruma, ila na vibwengo pia vipo, ndio kama huyu sasa.
 
Mkuu kuwa makini yawezekana anatumia triki uyo kukupiga virungu ili ajipatie riziki kupitia wewe wadada wa siku hizi ni majinamizi kabsa kuwa makini
Nadhani hilo ndilo litakuwa lengo lake
 
Hivi karibuni, nilipata mualiko kwa kamchepuko kangu, ambaye anadai ana ujauzito wangu.

Ikabidi niwe mzalendo na kuamua kufunga safari mpaka mkoa aliopo.

Baada ya kufika, nikatafuta eneo la malazi; nikapiga maji kidogo ili kuondoa uchovu, nikawa nimeagiza kinywani nakunywa taratibu hapo chumbani, huku nikimsubiri huyo mwali.

Baada ya muda nikapokea ujumbe wake mfupi, wa kutaka kujua sehemu niliyopo pamoja na chumba namba.

Baada ya kama nusu saa hivi, akawa amefika; nikiangalia tumbo lake naona limekuwa 'flat', nikajiuliza atakuwa amefyatua nini?

Basi tukawa tunazungumza; ila malalamiko yake mengi ni kutaka hela tu, mbaya zaidi alitaja mpaka kiasi; mi nikamwambia kwa sasa sina hicho kiasi, baadaa ya siku mbili nitakutumia.

Akawa mkorofi kweli, akawa hataki kunisikiliza; nikijaribu kumpatia 'romance' anapangua, baadaye ikabidi nitumie nguvu kidogo ingawa tulikuwa tunasukumana na hatukuweza kufanya lolote.

Ile naangalia tumbo vizuri, kumbe amelibana ili lisionekana; hapo hapo akili ikaniingia kichwani, huyu hayuko tayari kuwa na huu ujauzito.

Katika kuvutana vutana sana, nikaona isiwe shida, asije akapiga kelele nataka kumbaka; ile namuachia upenyo, akanyanyuka haraka nakufungua mlango na kutoka nje mpaka mapokezi, na kuanza kujisitiri vizuri ili aondoke.

Nampigia simu, anasema 'usinitafute tena na maamuzi ya huu ujauzito ninao mwenyewe'; mi nikamwambia sawa haina shida.

Baadaye ikabidi nitoke nje, ili nikabadilishe mazingira; napita pale mapokezi wakawa wananitazama kweli, nikasema kimoyo kimoyo sijui yule binti amewaambia kitu gani.

Niliporudi kulala nikawa sipati usingizi; ikabidi nitafute kampani huko 'online'; angalau aje anifariji kwa yaliyotokea.

Kusema kweli, si kila mwanamke ana sifa za kupewa ujauzito; najuta kupoteza mbegu zangu pale.​
Mm naona kajiongeza kaona we ndio huelewek,Kwanza ushasema n mchepuko ina maana huna malengo naye we.
 
Back
Top Bottom