Pape
JF-Expert Member
- Dec 11, 2008
- 5,487
- 83
kuna mshikaji wangu fulani ana mpenzi wake. Huyu jamaa alisota sana mpaka kumpata huyo mpenzi ikiwa ni pamoja na kupewa majibu ya kukatisha tamaa hapo mwanzoni. Siku ya siku ilipofika alikabidhiwa ufunguo! Kwasasa ni wapenzi kama wiki 3 hivi! mpenzi wake anasema anampenda sana jamaa ndio maana alikuwa anamchunguza kabla ya kumpa jibu la ndio!
Baada ya wiki moja huyu jamaa amegundua kwamba mpenzi wake ana wivu sana kwani hata jamaa akiwa anachati katika facebook, yahoo anahisi anachati na 'wanawake wengine'. jamaa amemweleza sana na kumtajia hata marafiki zake lakini bibie huyo anaona kama anaibiwa vile! Huyu jamaa ananyumba yake na mpenzie pia ananyumba yake! sasa mamaa anataka kila siku jamaa awe analala kwake (nyumbani kwa bibie) hata kama hawali tunda! Lengo sijui ni kutaka kuwa na uhakika kwamba anapata uhakika kwamba 'haibiwi'...
Jamaa yangu kwakweli anaona kama vile hii ni kero kwani hana nafasi hata ya kuongea na simu kwa uhuru, kuchati na washikaji na hata kutumia muda hapa JF...
Je, atumie mbinu gani kumwelewesha bibie kwani hata yeye anampenda sana na hataki kumpoteza!