America kukopa China

Nsera Ndawani

Senior Member
Joined
May 5, 2013
Posts
136
Reaction score
38
samahani sana
Nina shida ya uelewa kwenye jambo fulani.

Nina imani kwa kupitia kwenye hili jukwaa letu tukufu. Ambalo limesheheni mitazamo iliyo na upeo wa kutosha, ninaweza nikapata ufumbuzi.

Kwa sasa wataalam wanasema kuwa uchumi wa china unakaribia kuifikia nchi ya marekani. Na inasadikika kuwa marekani imekopa fedha nyingi sana kutoka china.

Na nchi ya china sarafu yake inaitwa Yuan ambayo inatumika pale china tuu. Lakini marekani sarafu yake ni Dollar na hii inatumika duniani kote. Sasa swali langu
Ni kwa nini marekani wanashindwa kutengeneza dollar nyingi na kuziuza na wakajipatia mahitaji yao yote?

Jee ni kitu gani marekani wanachokopa china? Ninaamini kuwa siyo tekinolojia.

Nina amini nitapata ushirikiano wa kutosha
 
Mimi siyo mchumi, lakini naamini kuchapisha noti nyingi ni kuporomosha uchumi kama ilivyotokea Zimbabwe! North Korea wanachapisha noti nyingi sana sa USD, ni superdollar ambazo zna ubora kuzidi hata za FR, wana uwezo wa kuchapisha nyingi watakavyo lakini uchumi wao bado uko dororo! again mimi siyo mchumi, wachumi wana lugha zao na maelezo mazuri wakija hapa watatusaidia!
 
Ninajua China inakopa US. Hilo la America kukopa China sijalisikia. Lakini China ina purchasing power kubwa sana japo hiyo haiifanyi iizidi marekani kiuchumi. Mfano GDP ya Marekani ni zaidi ya US$15 trillion, wakati China imezidi kidogo kwenye US$5 trillion. Ina maana GDP ya America yaizidi ya China mara tatu.
 

Well, usijali.

Ngoja nikupe walau basic knowledge!

Uchumi wa china kukaribiana na uchumi wa marekani.

Hii ni kwa kuangalia kitu kiitwacho GDP kwa nchi husika; ni masuala ya namba tu kwa ujumla wake.
Hivyo GDP ya china sasa inakaribia na GDP ya marekani;ndo kusema uchumi wa china unakaribiana na wa marekani.
Hapa mjadala bado ni mkali sana kwa kuwa:

GDP ya china ni kama dollar billion 13.4 na population yake ni km watu billion 1.3, wakati
GDP ya USA ni around dollar billion 16.8 huku population yake ni kama watu million 300.
Kwa hio ukaribu unaozungumziwa ni hizo dollar billion 13.4 na dollar billion 16.8 za GDP


Marekani kukopa China.

Yeah, hizi ni mbinu za kiuchumi. Kama unafuatilia hizi siasa za kiuchumi, pengine umewahi kusikia ni kwa nini China haitaki kutambulika kama one of the leading super power katika masuala ya kiuchumi. Kuna siri ndani yake. Lakini USA wanakopa China, ni sawa na kujaribu kujiuliza ni kwa nn Mkapa alibadilisha pesa; ni sawa na kujarbu kujiuliza kwa nini taifa lako linakopa kwa raia wake. Ni mada pana kidogo kwa mtu mdadisi anaependa kuona mambo katika jicho la tatu.

Naamini nimekutoa walau kutoka hatua a kwenda b.

Ahsante sana
 
Ni sawa tuwangoje wataalam
Watusaidie ili tupate ufahamu zaidi
 
Mkuu The dealer, GDP ya U.S unasema ni $ 16 billion na ya China ni $ 13 billion ? Una uhakika ?
 
GDP ya Us ni Trillion USD ndug,na sio billion USD
 

Asante sana
Jibu lako lina mashiko
 
china siku hizi inauza sana bidhaa kwa sababu pesa yake inathamani ndogo. wafanyabiashara wakiuza hizo bidhaa winapata dollar. sasa benki kuu ya china inachukua dollar za wafanyabiashara na kuwwapatia yuan. wafanyabiashara wa china wakitaka kuagiza vitu nje wanaenda kuchukua dollar benki kuu. lakini kwa vile china huuza sana kuliko kununua (trade surplus) inakuwa na dollar nyingi za ziada. zamani wakati dhahabu inatumika iliikuwa china wanapeleka hizo pesa marekani na kupewa dhahabu. siku hizi hizo pesa china huzitumia kuwekeza sehemu mbalimbali duniani na kinachobaki kinabaki kama deni kwa marekani.

ukisema uchapishe pesa kwa wingi unasababisha pesa zinakuwa nyingi kwenye mzunguko na kusababisha mfumuko wa bei. ila hii mbinu marekani wanaitumia kupunguza deni lao kwa china. yaani wanatengeneza dollar nyingi kwwa hiyo china anapata dollar nyingi sana. china akipata dollar nyingi inabidi atengeneze yuan nyingi za kuwalipa wafanyabiashara wanao mpa dollar. mwisho wa siku china kunakuwa na yuan nyingi na kussssababisha mfumko wa bei. mfumuko wa bei utasababisha china waongeze thamani ya pesa yao hivyo kupunguza uuzaji wa vitu vyao na deni la US litapungua.
 

Asante sana kwa kuniongezea ufahamu mkuu
 
Bahati mbaya ni kuwa masuala kama haya ya kiuchumi tulipaswa kujayajadili kwa mapana yake zaidi; lakini ukweli ni kwamba members wengi watajichimbia jukwaa la mmu na mengine kama hayo. Ila hii mada ni kubwa na ni nzuri kupita kawaida; ila bahati mbaya haitatendewa haki kwa uzito wake.

Watanzania madhalani kwa upande wao hawana hulka na silka ya kufanya mijadala ya kiuchumi na ndio maana ccm bado imeendelea kuaminika kama nambari wani; il hali imeshiriki kikamilifu kuua uchumi wa taifa kama taifa na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, yaani purchasing power kwa individuals!
 

Wrong Mkuu, US owes China about 1.5 trillion Dollars!
 
Sio kwamba marekani ina kopa kutoka china directly,,China ina miliki kiasi kikubwa cha USA treasury bonds kuliko nchi zingine(1.6 trillion $).China ina nunua sana US bonds kwa sababu zina aminika kuwa ni salama kuliko bond za nchi zingine.
Hilo ndio deni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…