"Amevunja kanuni na utaratibu wa chama,hatufai!kamati kuu imeridhia hatoteuliwa kuwa mtia Nia wa urais"!

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Wakuu

Nilipata wasaa wa kumtembelea kada mkongwe sana wa chama chetu Cha mapinduzi juzi huko isimani mkoani Iringa,tukapata wasaa wa kujadili mawili matatu juu ya mwenendo wa chama chetu kuelekea uchaguzi mkuu 2025!

"Kanuni tulizotumia mwaka 2015 wakati wa uteuzi wa hayati jpm ndizo tutazitumia 2025,uadilifu ndio msingi mkuu wa uteuzi was jina la mgombea wetu na SI vinginevyo!

Ugawaji wa Rushwa ya wazi na kuanza kampeni mapema plus ubadhirifu ndio kanuni pekee itakayotumika siku ya mkutano mkuu"

"Mtajwa ameshaonyesha dalili za kukiuka kanuni ameshagawa rushwa za pikipiki na bajaji zenye majina yake pia ameanza kampeni tangu mwaka 2021 Kwa kutamka hadharani atagombea na ushahidi wa wazi kabisa wa piki piki zenye picha yake ameshagawa hiyo ni rushwa ya uchaguzi na chama kimeamua kumuengua mapema kabisa,Mwambieni asijisumbue kwasababu amejiaharibia sifa zote za utia nia"

Nilipomuuliza kwamba desturi yetu inasema lazima ashike mara mbili na sio moja kwanini asiteuliwe!!?

"Ni Huwa anapewa mara mbili lakini amekiuka kanuni Kwa kutoa rushwa wazi wazi Tena bila kificho hiyo ni kuikosea CCM kama taasisi kongwe hapa nchini"

Bado natafakari Ndoto hii nilioiota usiku wa kuamkia leo!

Tusubiri tuone kitakachojiri 2025!
 
Ndoto kivipi wakati umeshatuambia ulipata wasaa wa kumtembelea yule jamaa wa jimboni Isimani, kule Iringa?

Anyway, all in all, huyo mama hafai tena kuwa kiongozi wa hili taifa, ana tuhuma nyingi zisizofaa mtu wa hadhi yake kuwa nazo.

Kuanzia zile za kule X zilizotolewa na Mange, rushwa ya wazi kama ulivyoonesha hapo juu, kushindwa kulinda rasilimali zetu, viburi kwa watendaji wake wanaojiona miungu watu wasiogusika hata wakosee vipi, ufisadi miongoni mwa wasaidizi wake na yeye mwenyewe..

Simply amefeli pakubwa kuliongoza hili taifa, ndio maana awamu hii chawa wana sauti zaidi ya mtawala, hii maana yake mtawala hajitambui, hajui anachofanya, wala hawezi kutolea maelezo tuhuma zinazoikabili serikali yake, anaongoza taifa kwa kubahatisha ameamua kujiita chura.
 
Ukilala kwenye jumba bovu lazma unakuwa na ndoto kama hizi maana ni uhalisia wa unakolala na mwenye kukabidhiwa nyuma afanye maboresho katoa bati Katia paa la mifuko ,Kuta nazo zimetoboka ,kwa jirani Kuna unafuu ......endelea kuskiza hii nyimbo ukiwa usingizini
 
Wazee walikabidhiwa hii nchi wapo ,na viongozi wa dini wapo Mimi na wewe tupo tunafeli wapi sasa
 
Hata Mimi naona,ngoja nitoe mifuko niweke nyasi walau nitaota nimeshinda jackpot!
 
Ninachokijua mpaka sasa kama Mwenyezi Mungu akimlinda mpaka 2025 , Madam President atapitidhwa kwa kishindo na CCM na atashinda kwa kishindo. Jukumu la CCM ni kulinda legacy ya ushindi ya 2020 na kuweka mpya chini ya Dkt.Samia asiyekubaliana na hilo alambe wembe
 
Legacy ilisababisha hadi tukarudi kati sio!?unataia yajirudie Yale ili turudishwe kati tena!!?

Kuwa makini!
 
Rais nchi hii yuko juu ya hata hao wazee wa ccm. Hakuna uwezo wa kumtoa kwa mizengwe maana ccm yote kama chama inategemea madaraka hayo ya urais kubaki madarakani.
Ulichoandika kingekuwa na ukweli, 2015 rais angekuwa Membe. Huyo ndiye alikuwa chaguo la rais Kikwete, wajumbe wakasema hapana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…