DOKEZO Amewasilisha Polisi malalamiko ya ndugu yake kuuawa lakini Askari wa Kituo cha Polisi Kibaha wanamzungusha tu

DOKEZO Amewasilisha Polisi malalamiko ya ndugu yake kuuawa lakini Askari wa Kituo cha Polisi Kibaha wanamzungusha tu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu kwanza Pole sana kwa msiba

Pili umejuaje kama marehemu alipigiwa simu akaenda na wakamtaka awalipe laki 5 na wakati unasema walishamnyang'anya simu?

Kabla ya kufa marehemu alikuelezea mtiririko wa matukio yote?
 
Pole Kwa changamoto zinazokukabili maana umempoteza ndugu na Kwa kuwa huna koneksheni umeshindwa kupata haki.Jaribu kuwasiliana na igp Kwa namba hizo pengine unaweza kusikiliza.
Screenshot_20230919-111305.jpg
 
Bashite kama Bashite mimi nimebaki ndugu mtazamaji tu kwa mbali kwenye kaa kona.

Moyo wa mtu kichaka siwezi juu wewe na Bashite nini kinaendelea
😂😂😂 huo ni uovu mkuu...unanikosea sana
 
0699998899 mpigie IGP now atakusikiliza na ni moja kati ya mapolisi wenye utu na ubinadamu.
 
Hao wapelelezi kwenye vituo vya polisi mi naonaga ni wamchongo tu.....si professional na hawapo kwa ajili ya kazi bali pesa mbele
That's it sasa mtu anakupa tips na bado unamtaka amlete eti mtu aliyeshudia, kazi ya upelelezi ni nini? Nyenzo wanapewa elimu wanapewa zaidi ya yote umepewa na tips, hawa askari noma sana.
 
R I p
Lakini wengi mmesahau kipengere cha wizi wa kokoto, hapo kuna kitu
 
poleni sana, ila hapo kwenye maelezo kuwa walidai 500,000/= naye akasema ana 50,000/= yametolewa na nani? maana kwa mtazamo wangu hiyo ilikuwa sehemu nzuri sana ya kuanzia uchunguzi juu ya mauaji hayo.
note: samahani kama nitakuwa nimekukwaza kwa swali hilo.
 
Wame shiba na vitambi vyao hadi,watu kama Hamza waamke awatie shaba ndo wana shtuka
 
Askari wa siku hizi wamekuwa wazembe , hawataki kufanya majukumu Yao kabisa, sasa kazi ya kumkamata muhalifu ni ya raia au Askari?
Nazani tatizo liko kwenye budget, kuna vituo vingine vinajiendesha vyenyewe,ndiyo maana huwa wanataka uchangie kiasi flani cha pesa, labda utaambiwa weka mafuta kwa defender ili akakamatwe muhalifu wako! Kitaalamu tunasema unachangia uchakavu,au tunagawana umasikini!!
 
Polisi wote wapo hivyo hivyo tu.

Na ndiyo wanaohamasisha haya matukio yaongezeke maana hakuna ufuatiliaji.

Hapo mbona ni rahisi tu kuwapata wahusika,namba iliyowasiliana na marehemu kabla ya tukio si inafahamika.
 
Tarehe 24/01/2024 Ndugu Hamis Athumani Mkazi wa eneo la Mashamba Pori, Kibaha Mkoani Pwani aliuliwa kwa kupigwa na machepe.

Siku ya tukio Marehemu alikuwa nyumbani kwake eneo la Mashamba Pori akapigiwa simu katika simu yake no. 0654281507, akaelekezwa aende eneo la Pangani ambalo ni kama Kilometa 4 kutoka nyumbani, alifanya hivyo kwa kuwa waliomuita ni watu anaofahamiana nao na anafanya nao kazi hasa za vibarua.

Alipofika eneo hilo la Pangani akawakuta Watu nane wakati huo tayari kulikuwa na Viroba nane vya kokoto pembeni, yasemeka walianza kuzozana huku watu hao wakimtaka atoe Shilingi Laki Tano ambayo hakuwa nayo na akawasihi wasimshambulie huku akidai mfukoni ana Sh 50,000 tu.

Akawasisitiza kuwa kama wanataka hizo Laki Tano wampigie simu Mama yake kwa simu yake ambayo walikuwa wameshamnyang'anya lakini hata hivyo walikataa na kumshambulia hadi kufa.

Watu walivyoanza kujitokeza baada ya kusikia purukushani, wale jamaa wakadai Hamis ni mwizi wa Kokoto na wamemkuta anaiba, Wananchi kusikia hivyo wakiwemo Bodaboda wakatoa Petrol kwenye Pikipiki zao na kuanza kumbabua kwa Moto.

Mwili Marehemu ulikaa hapo kuanzia alivyouliwa Saa 4 Asubuhi hadi Saa Tisa Alasiri ndipo Askari Polisi wa Wilaya ya Kibaha walipofika eneo hilo kuchukua Mwili na kuupeleka Mochwari.

Jambo la kushangaza kesi iliyofunguliwa hapo Kibaha ni kosa la kujeruhi KBH/IR/333/2024 ya tarehe 24/01/2024, Mpelelezi SGT Ombeni wa Ofisi ya OC CID Kibaha na Mkaguzi wa tukio hilo alikuwa Insp Peter wa Kituo cha Polisi Kibaha.

Kaka wa Marehemu Salehe Athumani mwenye simu namba 0712249269 alifika baada ya kupata taarifa na alikabidhiwa mwili wa ndugu yake tarehe 25/01/2024 na Mpelelezi SGT Ombeni kwa ajili ya kwenda kumhifadhi mpendwa wao.

Baada ya hapo alianza kufuatilia ikiwa ni pamoja na kufika nyumbani kwa Marehemu ambapo alipata taarifa nyingi kuhusiana na kifo cha mdogo wake na kukugundua kuwa hakua mwizi bali kulikuwa na visa vya wivu.

Akaenda hadi Kituo cha Polisi Kibaha kumuona Mpelelezi SGT Ombeni na baada ya kumuekeza yote kuhusiana na kifo cha Mdogo wake pamoja na kutaja hadi majina ya washukiwa waliomuua mdogo wake kuwa ni Watu ambao walikuwa wakishikiana kwenye kazi mbalimbali kwa kuwa marehemu alikuwa Fundi na wauaji mara nyingi walikua wasaidizi wake.

Licha ya maelezo yote hayo bado Mpelelezi SGT Ombeni alimuelekeza aende akawalete Watu walioshudia wakati wanamuua Mdogo wake lakini hata kabla ya hapo kuna mtu alielekezwa aende akaandike maelezo alichoshuhudia lakini inadaiwa baada ya hapa alitakiwa kutorudi tena pale kituoni na wala kutoeleza alichoongea kule Polisi.

SGT Ombeni akamuelekeza kaka wa marehemu kwenda kwa OC CID, akafanya hivyo kwa kwenda kwa Mkuu wa Upelelezi, akamueleza kila kitu anachokijua na kumtajia majina ya washukiwa wa mauaji, nae akamwambia aondoke akatafute shuhuda wa tukio ambaye yupo tayari kutoa maelezo.

Kufikia hatua hiyo ndugu wa marehemu hakuwa na la kufanya tena zaidi ya kutafuta usafiri wa kurudi Kijijini kwake Makanya Wilaya ya Same.

Hilo ndio Jeshi la Polisi Tanzania.
Pamoja na maelezo mazuri,kuna tatizo sehemu.Wakutane tu na kuanza kuzozana bila chanzo?Kuua ni kosa.Wauaji wasakwe.
 
Back
Top Bottom