VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Scenario 1: Lissu ameshinda Urais wa Tanzania. Anaunda Serikali. CCM ina wingi wa Wabunge. Inatoa Waziri Mkuu na Mawaziri wengi. Serikali ya Lissu itapelekeshwa na chama chetu tutakavyo na kukistawisha chama kuelekea 2025. CCM itashinda kwa kishindo mwaka 2025.
Scenario 2: Lissu hashindi Urais. Hawi Mbunge. Anabaki kama Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA. Anabaki kuwa mwanasiasa wa CHADEMA kukitangaza, kukistawisha na kukipigania chama chake akiutumia Uanasheria wake.
Ataungana na John Mnyika ambaye naye pia hatakuwa Mbunge. CHADEMA itastawi, CCM itasinyaa. Hakika, Lissu na Mnyika wataisambaratisha CCM. Mwaka 2025, CHADEMA haitazuilika katika kuchukua Serikali.
Ni heri Lissu na Mnyika watingwe na Urais na Ubunge. Wakiwa wanasiasa wa kichama zaidi, CCM itapotea kwenye ramani za siasa Tanzania mwaka 2025.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kigoma).