Elections 2015 Amini Usiamini, Kama Mwalimu Angekuwa Hai Hadi Leo!, Angemsupport Edward Lowassa!.

Elections 2015 Amini Usiamini, Kama Mwalimu Angekuwa Hai Hadi Leo!, Angemsupport Edward Lowassa!.

Wanabodi,

Wakati Watanzania tukijiandaa kukumbuka kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwallimu Nyerere, naomba kutoa angalizo la kuizuia kumbukumbu hiyo isitumike vibaya kuupotosha umma eti kuna watu Mwalimu aliwakataa!, yes anaweza kuwa aliwakataa wakati ule ile kama angekuwa hai hadi leo, angewakubali sana tuu!.

Kiumri mimi ni mtu mzima nitaitafuta 50 kwa karibu!.

Kikazi, mimi ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea!. Kwa mara ya kwanza kuingia newsroom ilikuwa ni mwaka 1990 ndani ya chumba cha habari cha gazeti la serikali Daily News, hivyo kama ningekuwa bado niko kazini mpaka leo, mwaka huu ningesherehekea miaka 25 ya uandishi wa habari!.

Katika kipindi hicho, Mwalimu Nyerere alikuwa ameishastaafu na sikuwahi kukosa kuhudhuria press conference yake yoyote, hivyo Mwalimu ninamfahamu fika!. Tena ilitokea, nadhani mimi ndio mwandishi wa habari wa Tanzania kufanya mahojiano ya mwisho na Mwalimu, ambayo niliyafanya mwaka 1998, katika ukumbi wa The Bundes House, katika mji wa Bern Nchini Uswisi, baada ya hapo alianza kuugua hadi Mwenyeenzi Mungu alipomuita kumpumzisha!, hivyo Mwalimu Nyerere huyu ninayemzungumza hapa, ni Mwalimu ninayemfahamu kwa kuzungumza naye ana kwa ana na sio Mwalimu wa kumsikia, kumuona au kuhadithiwa!.

Katika ule mkutano wake na waandishi wa habari Katika Hoteli ya Kilimanjaro, alipokuwa anazungumzia kuuzwa kwa benki ya NBC, Mwalimu alitokwa machozi kwa uchungu!, leo angekuwepo na kusikia sio tena kuuzwa kwa benki tuu bali viongozi wa umma, wenye uwezo wa kujenga nyumba zao, na baadhi yao wenye majumba yao tayari, lakini wakayachukua majumba ya umma na kujigawia bure, kwa kuweka vijisenti kidogo vya kudanganyia!, leo mtekelezaji wa uharamia huo, ambaye sio tuu alijigawia pande nono, bali pia aliwagawia na vimada wake kadhaa!, jambo kama hili, Mwalimu asingelikubali!.

Nakiri nimekuwa inspired kuandika bandiko hili, kutokana na swali la mwana jf huyu,
Mkuu Shemeji,Mikael P Awedak amini usiamini, kama Mwalimu angekuwa hai hadi leo, angejiunga na Lowassa!.

Ni Mwalimu ndie aliyesema upinzani wa kweli, utatoka CCM!, this is that time Mwalimu aliyoisemea!.

Mimi ni muumini wa life after life!, Mwalimu huko aliko anampigania Lowassa!.

Ni Mwalimu ndie aliyesema, watu wanataka mabadiliko, wakiyakosa ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM!.

Pasco
Kama mwandishi mbobezi, hebu tuambie, unavyomfahamu mwalimu angekubaliana na suala la bandari na mkataba wa vipengele vile. Au tungesikia kujiuzulu kila kona?
 
Wanabodi,

Katika ule mkutano wake na waandishi wa habari Katika Hoteli ya Kilimanjaro, alipokuwa anazungumzia kuuzwa kwa benki ya NBC, Mwalimu alitokwa machozi kwa uchungu!, leo angekuwepo na kusikia sio tena kuuzwa kwa benki tuu bali viongozi wa umma, wenye uwezo wa kujenga nyumba zao, na baadhi yao wenye majumba yao tayari, lakini wakayachukua majumba ya umma na kujigawia bure, kwa kuweka vijisenti kidogo vya kudanganyia!, leo mtekelezaji wa uharamia huo, ambaye sio tuu alijigawia pande nono, bali pia aliwagawia na ndugu zake, rafiki zake, jamaa zake, hadi vimada wake kadhaa!, jambo kama hili, Mwalimu angekuwepo, asingelikubali!, angemchagua Lowassa!.

Pasco

Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 

Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
Nani basi aandike tribute nzito iliyoshiba ? Anzia Lowasacwa AICC hafi huyu wa CDM na kurudi CCM....? Naomba sana P tafakari andika Tribute ya ENL....sidhani JK atakuwa muungwana kuandika na kusema yoote....andika uta edit atayosema JK najua unafiki...pale Monduli....tafadhaliii
 
Back
Top Bottom