Amini usiamini! Nimeokota Tsh milioni 6

Amini usiamini! Nimeokota Tsh milioni 6

Hongera mdau,Rizki huletwa na Muumba kwa staili tofauti,na Muumba akitaka kukupa rizki hakuandikii BARUA
Siyo siyo riziki, kuna mmiliki ameathirika kwa kupoteza hiyo fedha. Tangaza ili umrudishie mmiliki wake, rudisha haraka.
 
Siyo siyo riziki, kuna mmiliki ameathirika kwa kupoteza hiyo fedha. Tangaza ili umrudishie mmiliki wake, rudisha haraka.
Unaweza ukatangaza,lakini mtangazaji uweke masharti magumu sana,maana huenda ukampa mtu ambaye si mwenye mali,je ulishawah kufanya hivyo?katika mazingira gani?mfano miskitini utakuta mtu amepoteza labda SAA,Imam anapotangaza aidha anaweza kusema saa ila hataji aina ya saa na rangi ili kubaini mpotezaji ni yeye au lah,na hata kuulizwa uliiacha wapi?na pia wapo wanaopoteza wallet,pia yatawekwa mafumbo kadhaa ili muhusika athibitishe.
Swala la hizo pesa,labda umsaidie muhsika akatangazie wapi?nani wa kumpa jukumu la kutangaza?na mambo kama hayo,ili mwenye mali yake wa kweli aipate,vinginevyo jamaa atumie tu pesa hakuna namna
 
Ilikuwa hivi:

Jirani na ninapoishi kuna eneo limetengwa na Manispaa kwa ajili ya kuhifadhi takataka kwa muda kabla gari la Manispaa halijaja kubeba taka hizo.

Wakazi wengi wa mtaa wetu huona uvivu kwenda kumwaga taka ktk chemba hiyo iliyotengwa, badala yake husubiri usiku mwingi kuja kumwaga taka zao jirani kabisa na nyumba yangu.

Asubuhi ilipofika, nikaamka na kukuta furushi la taka jirani na kwangu.

Nikaghadhibika sana

Nikaamua kulibeba furushi hilo na kulipeleka dampo (chemba). Wakati nalikokota, furushi lile likanaswa na kipande cha mti, likapasuka na uchafu ukasambaa.

Hamadi!!!!

Nilichokiona, sikuamini. Nilipigwa butwaa. Baada ya akili kuwa Sawa, nikainama na kuokota na kukimbilia nyumbani, tena chumbani kwangu.

Nimezihesabu. Zipo Tsh 6,000,000 (milioni 6).
Macho kuona mkuu
 
Hongera mkuu, ndio malipo yako ya kufanya usafi.
 
Mtoa post Ana roho ya ushawishi. Anahamasisha watu wachakurechakure majalalani. Hicho kipaji angekitumia kuuza bidhaa za Forever Living ingekuwa poa.
 
Hongera mdau,Rizki huletwa na Muumba kwa staili tofauti,na Muumba akitaka kukupa rizki hakuandikii BARUA

Kwa kweli pana jamaa flan hivi nae aliolota pembe ya faru akauza 130Milioni...kama ujuavyo banki zetu hizi ukiwa na pesa mingi husumbua saana kila siku wanamhojo wapi kapata pesa nyingi hivyooo!!!
 
Kwa kweli pana jamaa flan hivi nae aliolota pembe ya faru akauza 130Milioni...kama ujuavyo banki zetu hizi ukiwa na pesa mingi husumbua saana kila siku wanamhojo wapi kapata pesa nyingi hivyooo!!!
Ni kweli nao hubanwa na sheria za BOT ndo maana wanamuuliza sana hivo,ila huwez kukosa jibu,sasa niokote pembe la faru halafu nipeleke maliasili si nitakua chizi jamani
 
Back
Top Bottom