Amini usiamini, Tanzania hadi sasa ina flyover mbili (2) tu zinazofanya kazi rasmi

Amini usiamini, Tanzania hadi sasa ina flyover mbili (2) tu zinazofanya kazi rasmi

Maana kwanza nicheke, hivi hii nchi tunaambiwaga ina watu milion 60 ni kweli au ni nadharia?! Yaani flyover 1 kwa watu milioni 30?! Hivi hii inaingia akilini kweli?!

Hebu tusubiri Sensa tuone, hadi majibu ya Sensa yatoke ndio ndio nitaamini
We umeona kua na flyover nyingi ndio kua na maendeleo
 
Hamnaga shukrani alikuwa anatengeneza flyover lakini hakuna ajira mpya Wala kupandisha mishahara mkasema maendeleo ya vitu maisha magumu kaja anataka maendeleo ya watu Bado mnaongeaaaa
Huyu mama anataka kufurahisha watu, sio kuleta maendeleo.

Maendeleo hayawezi kuja kwa kuchekeana chekeana. Wazungu hawakufika hapo kwa kuchekeana, wamwpigana vita nyingi sana kuwekana sawa.

Sisi Tanzania tunataka kuchekeana, mara mama asamehe wasiolipa kodi, sasa unasamehe watu wasilipe kodi wewe nchi utaiendeshaje, kwa kukopa na kuomba misaada?

Hakuna maendeleo yamewahi kuletwa hapa Duniani kwa misaada na mikopo. Hakuna.

Hii nchi tuna bahati mbaya sana.
 
Maana kwanza nicheke, hivi hii nchi tunaambiwaga ina watu milion 60 ni kweli au ni nadharia? Yaani flyover 1 kwa watu milioni 30?! Hivi hii inaingia akilini kweli?

Hebu tusubiri Sensa tuone, hadi majibu ya Sensa yatoke ndio ndio nitaamini
Kwan watatoa majibu ya sensa Sasa. Wakitoa niite mbwa nimekaa hapo

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Tumshukuru sana mzalendo magufuli aliip a mbania Tanzania yetu.Naamini angekuwepo nchi ingetapakaa flyover kila mahali.Maana toka atutoke hakuna flyover mpya iliyobuniwa na awamu hii mpya zaidi tu ya alizoziacha ambazo zingine zinamaliziwa kwa sasa japo za sasa zimechakachuliwa.Yaani hazina mvuto na ubora.
 
Back
Top Bottom